SZA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtumiaji:Nataliekarunga)
Ziara ya SZA CTRL Toronto 2017

Solána Imani Rowe (anayejulikana kama SZA hutamkwa /sɪzə/; alizaliwa 8 Novemba 1989) ni mwimbaji wa R&B na mtunzi wa nyimbo kutoka Marekani. Alipata umaarufu kutokana na kutoa albamu zake ndogo, See.SZA.Run(2012) na S(2013). Baada ya kutoa albamu hizi ndogo, alisaini mkataba wa rekodi na Top Dawg Entertainment. Albamu yake ndogo ya tatu Z (2014).[1]

SZA alitoa albamu yake ya kwanza ya studio CTRL (2017) baada ya kusaini mkataba wa pamoja wa rekodi na RCA records. SZA albamu ya pili ilitumia wiki kumi kwenye ubao wa matangazo 200 na alipata mafanikio mengi. Nyimbo kumi bora “Good Days”, “I Hate U”, “Nobody Gets Me” na “Snooze”. SZA alipata wimbo wake wa kwanza kwenye ubao moto 100 na “Kill Bill”.

SZA amepokea sifa nyingi katika kazi yake kama Tuzo ya Grammy nne, Tuzo ya Brit, Tuzo ya Muziki ya Marekani, Tuzo ya ubao wa matangazo ya wanamke mbilli na mwanamke wa mwaka. Kama mtunzi wa nyimbo, ameandika nyimbo na Nicki Minaj, Travis Scott na Rihanna.[2]

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Solána Imani Rowe alizaliwa mnamo tarehe 8 Novemba 1989. Alizaliwa katika jiji la St. Louis, Missouri. SZA alilelewa mji wa Maplewood, New Jersey. Baba yake alikuwa mtayarishaji mkuu wa CNN na Mama yake kufanya kazi katika AT&T. Rowe ana dada. Dada yake anaitwa Panya Jamila. Mama yake ni mkristo na Baba yake ni muislamu. Rowe alilelewa muislamu na anaendelea mazoezi uislamu. [3]

Akiwa mtoto, alisoma shule ya msingi ya Kiislamu. Rowe alihudhuria Columbia High School katika mji wa Maplewood na Jimbo la New Jersey, ambapo alicheza michezo kama mazoezi ya viungo na ushangiliaji. Rowe alihudhuria Chuo Kikuu cha Jimbo la delaware kusoma biolojia ya baharini.

Rowe alipata jina lake la jukwaa toka rapa RZA wa Wu tang Clan. S maana yake ni mwokozi, Z maane yake ni Zig Zag na A maane yake ni Allah.

Kazi Safi[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 9 Juni, 2017 SZA  alitoa albamu yake ya kwanza ya studio Ctrl, Ctrl ilipata nafasi ya tatu kwenye Billboard 200 ya Marekani. Wimbo wake “Love Galore” ulifikia kilele cha 40 bora kwenye Billboard Hot 100 chati. Ctrl iliorodheshwa kama albamu bora zaidi ya 2017. Kutoka Agosti 2017 hadi Februari 2018 SZA alikwenda kutangaza albamu na maonyesho kote Marekani. Tarehe 9 Desemba, 2022 SZA alitoa albamu yake ya pili ya studio SOS, albamu ilikaa wiki zake saba za kwanza juu ya Billboard 200. SZA ameigiza katika onyesho “Insecure” kama Latoya kwa sehemu moja [4]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

  • Crtl (2017)
  • SOS (2022)

Ziara[hariri | hariri chanzo]

Mtumbuizaji mkuu

  • Crtl the Tour (2017-2018)
  • SOS Tour (2023-2024)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "You Don't Know SZA Yet, But You Will". HuffPost (kwa Kiingereza). 2014-07-23. Iliwekwa mnamo 2024-04-27. 
  2. Jem Aswad (2023-11-29). "SZA, Variety’s Hitmaker of the Year, Unpacks ‘SOS,’ Her 9 Grammy Noms, and Says ‘F— You’ to Song Leakers". Variety (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-04-27. 
  3. Danny Schwartz (2017-06-14). "Everything You Need To Know About SZA". HotNewHipHop (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-27. 
  4. HipHopDX- https://hiphopdx.com (2017-06-19). "Hip Hop Album Sales: SZA's "CTRL" Debuts On Billboard 200". HipHopDX (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-27.