Nenda kwa yaliyomo

Kukwama kwa leba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
mchoro wa ulemavu wa Pelvis-angular ya kike ambayo inaweza kusababisha leba pingamizi
Obstructed labour
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuObstetrics and gynaecology Edit this on Wikidata
DiseasesDB4025
eMedicinemed/3280
MeSHD004420

Kukwama kwa leba, hali ambayo pia hujulikana kamadistosia ya leba, ni wakati ambapo, hata ikiwa uterasi ina mikazo ya kawaida, mtoto hatoki kupitia pelvisi wakati wa kuzaliwa kwa sababu ya kufungika.[1] Kutatizika kwa mtoto hujumuisha ukosefu wa oksijeni ya kutosha hali inayoweza kusababisha kifo. Hali hii huongeza hatari kwa mama ya kupata maambukizi, kupasuka kwa uterasi, au [[kuvuja damu baada ya kuzaa].[2] Matatizo ya muda mrefu ya mama yanajumuisha fistula ya uzazi. Kukwama kwa leba huaminika kusababisha leba ya muda mrefu, wakati awamu tendeti ya leba inapozaidi saa kumi na mbili.[1]

Visababishi na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Visababisishi vikuu vya kukwama kwa leba hujumuisha: mtoto mkubwa zaidi au aliyelala kwa namna mbaya tumboni, pelvisi ndogo, na matatizo katika njia ya uzazi. Hali za kulala tumboni zisizo za kawaida hujumuisha distosia ya bega ambapo bega la upande wa juu halipitii chini ya fupa la uzazi kwa urahisi.[1] Vipengele vya hatari vya pelvisi ndogo hujumuisha utapiamlo na ukosefu wa miale ya jua hivyo kusababisha ukosefu wa vitamini D.[3] Hali hii hutokea mara nyingi katika ubaleghe kwa sababu mara nyingi pelvisi huwa haijakamilika kukua.[2] Matatizo kwenye njia ya uzazi hujumuisha uke na msamba mwembamba, hali inayoweza kusababishwa na ukekektaji au tyuma.[1] Patografu mara nyingi hutumika kufuatilia jinsi leba inavyoendelea na kutambua matatizo.[2] Hii, pamoja na uchunguzi wa kimwili unaweza kutambua leba iliyokwama.[4]

Udhibiti na epidemiolojia

[hariri | hariri chanzo]

Matibabu ya leba yanaweza kuhitaji kuzaa kwa njia ya upasuaji au kuvuta vipande vilivyobakia na hata pia upasuaji wa kufungua simfisisi ya uzazi. Hatua nyingine hujumuisha: kuhakikisha mwili wa mwanamke una maji ya kutosha na antibiotiki ikiwa tando zilipasuka zaidi ya saa 18 zilizopita.[5] Barani Afrika na Asia, kukwama kwa leba hutokea kwa wanawake wawili hadi watano wanaozaa.[6] Mwaka wa 2013, hali hii ilisababisha vifo 19,000 tofauti na vifo 29,000 mwaka wa 1990 (takriban 8% ya visa vyote vyavifo vinavyohusiana na ujauzito).[7][1] Vifo vingi vinavyosababishwa na hali hii hutokea katika mataifa yanayoendelea.[2]

References

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Education material for teachers of midwifery : midwifery education modules (PDF) (tol. la 2nd ed.). Geneva [Switzerland]: World Health Organisation. 2008. ku. 17–36. ISBN 9789241546669. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-02-21. Iliwekwa mnamo 2015-08-17. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 Neilson, JP; Lavender, T; Quenby, S; Wray, S (2003). "Obstructed labour". British medical bulletin. 67: 191–204. PMID 14711764.
  3. Education material for teachers of midwifery : midwifery education modules (PDF) (tol. la 2nd ed.). Geneva [Switzerland]: World Health Organisation. 2008. ku. 38–44. ISBN 9789241546669. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-02-21. Iliwekwa mnamo 2015-08-17. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  4. Education material for teachers of midwifery : midwifery education modules (PDF) (tol. la 2nd ed.). Geneva [Switzerland]: World Health Organisation. 2008. ku. 45–52. ISBN 9789241546669. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-02-21. Iliwekwa mnamo 2015-08-17. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  5. Education material for teachers of midwifery : midwifery education modules (PDF) (tol. la 2nd ed.). Geneva [Switzerland]: World Health Organisation. 2008. ku. 89–104. ISBN 9789241546669. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-02-21. Iliwekwa mnamo 2015-08-17. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  6. Usha, Krishna (2004). Pregnancy at risk : current concepts. New Delhi: Jaypee Bros. uk. 451. ISBN 9788171798261.
  7. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 Desemba 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013". Lancet. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2. PMID 25530442. {{cite journal}}: |first1= has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)