Nenda kwa yaliyomo

Google Play

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Logo ya Google Play.

Google Play ni jukwaa la kujipatia programu au apps za mfumo wa uendeshaji wa Google Android. Ni duka la mtandaoni kwa ajili ya muziki, vitabu, filamu na progamu zote za Android.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kabla kuanzishwa kwa Google Play, kulikuwa na maduka ma-4 tofauti ya Google. Kwa leo maduka haya yote yamefungamishwa:

  • Google Music--kipengele hiki huwa na muziki. Huweza ukapata kwamba kina zaidi ya miziki milioni arobainne.
  • Google Books--kipengele hiki huwa na vitabu dijitali yaani ebooks.
  • Google Movies-- hiki huwa na sinema na pia programu za runinga zinazopendwa sana na zilizo za kuuzwa au kukodishwa.
  • Android Market--huwa na programu za android
  • Google News--Kipengele hiki huwa na majalada na magazeti ya habari

Historia ya Google Play

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 7 Machi, 2012, Google walitangaza ya kwamba wataziweka huduma hizi zote 4 katika sehemu moja, Google Play.

Programu zilizoko katika Google play huwa za kulipa ama za kuchukua bure. Programu hizi huweza kupakuliwa kwa simu au kifaa kinachotumia mfumo wa Android kama vile Tablet.

Android Market

[hariri | hariri chanzo]

Android Market ilianzishwa punde baada ya Apple App Store mnamo tarehe 22 Oktoba 2008.

Njia za kulipa katika Google Play

[hariri | hariri chanzo]

Kupata programu au vipengele vilivyotajwa hapo juu, mtumiaji afaa kulipa kwa kutumia njia zifuatazo:

  1. Paypal au malipo kwa kutumia kadi ya debit au ya mikopo (credit card)
  2. Gift cards: Kutoka mwaka wa 2012 kulikokuwa na fununu kuwa kuna Google play gift cards, kampuni ya Google iliamua kuweka hizi gift cards kirasmi. Kwa sasa, waweza kupata gift cards kwa zaidi ya nchi 20.
  3. Subscriptions: Pia kuna kulipa kwa subscriptions ambapo mtumiaji apata kutumia programu kwa mwezi au wakati fulani hadi wakati ule uishe alipe tena
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.