Utambuzi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
This article was created in relation to Afrocuration project.
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:16, 6 Juni 2020

Kwenye matibabu, utambuzi wa matibabu ni mchakato wa kuamua ni ugonjwa gani au hali zinazoelezea dalili na ishara alizonazo mtu. Mara nyingi hali hii uelezewa kuwa ni utambuzi uliowekwa wazi kitabibu. Taarifa zinazotakiwa wakati wa utambuzi ni zile zilikusanywa kutokana na uchunguzi wa kimwili na historia ya muhusika anayetaka huduma ya afya. Mara nyingi utambuzi mmoja au zaidi hufanywa wakati wa mchakato wa utambuzi kama vile vipimo vya matitabu. Wakati mwingine utambuzi baada ya kifo hutambuliwa kama utambuzi wa kitabibu. Utambuzi mara nyingi huwa na changamoto, kwa sababu dalili na ishara siyo maalumu. Kwa mfano wekundu kwenye ngozi, unaweza kuwa ni dalili ya matatizo mbalimbali hivyo haiwezi kumjulisha mtoa huduma ya afya tatizo ni nini.

Utaratibu

Vipengele vya jumla ambavyo vipo kwenye mchakato wa utambuzi kwenye njia mbali mbali zilizopo:

  • ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za mgonjwa, ambazo zitahusisha maswali ya historia ya matibabu (hasa toka kwa watu mbalimbali na pia toka kwa watu wa karibu na mgonjwa), uchunguzi wa mwili na vipimo vya utambuzi
  • Kipimo cha utambuzi ni aina mbalimbali za utambuzi wa matibabu unaofanywa kusaidia utambuzi au ugunduzi wa ugonjwa. Vipimo vya utambuzi hutumika pia katika utoaji wa taarifa za utambuzi za watu wenye gonjwa lililopo.
  • Mchakato wa majibu, na utafiti wa matokeo mengine. Ushauri na wataalamu wengine katika nyanja hiyo unaweza tafutwa.

Kuna njia mbalimbali au mbinu zinazoweza kutumika katika mchakato wa utambuzi, zikiwemo kufanya utambuzi tofauti au kufuata Algorithms ya matibabu yaani en:medical algorithms.[1] Kiuhalisia mchakato wa utambuzi unaweza kuhusisha vipengele vya njia nyingine.[2]

Utambuzi wa Covid-19

Jinsi ya kupima COVID-19 katika picha

Maambukizi ya Korona COVID-19 yanaweza kutolewa kwa muda kwa kuangalia dalili ingawa uthibitisho wa mwisho ni kupitia (rRT-PCR) yaani en:Reverse transcription polymerase chain reaction (rRT-PCR) ya majimaji yaliyoathirika au kwa picha za CT. Utafiti unaolinganisha PCR kwa CT uliofanyika Wuhan unashauri CT ni wa maana na nyeti zaidi ya PCR, ingawa haiko maalumu yenye vipengele vinavyoingilianq kwenye picha zake nyingi na aina nyingine ya muendelezo wa ugonjwa wa pumu yaani pneumonias. Kuanzia Machi 2020, Chuo cha Radiologia cha Marekani yaani the American College of Radiology kinashauri kuwa "CT isitumike kwenye uchunguzi wa awali kwenye utambuzi wa COVID-19".

Upimaji wa virusi

Shirika la kimataifabla afya duniani yaani WHO ilichapisha RNA mbalimbali za protokali ya upimaji wa kirusi cha korona COVID-19, chapisho la kwanza lilitoka tarehe 17 ya Januari.[3] Kipimo hiki kimetumia kipimo halisi cha rRT-PCR yaani en:reverse transcription polymerase chain reaction (rRT-PCR).[4] Matokeo yake mengi hitoka baada ya masaa machache hadi siku kadhaa.[5] Kwa ujumla kipimo hiki hupimwa toka kwenye en:nasopharyngeal swab kupitia koo ambako throat swab inaweza kutumika.[6]

Maabara nyingi na kampuni zinazotengeneza vipimo vya vserological tests, ambavyo hutambua which antibodi yaani antibodies. Hadi kuanzia tarehe 6 Aprili 2020 hakuna njia hata moja imethibitishwa kutosheleza na kuruhusiwa kwa matumizi ya wengi/zaidi. Marekani kipimo cha serological kilichoanzishwa na Cellex kimeithinishwa kwa matumizi ya dharura kwa maabara zilizosajiliwa pekee.

Picha ya CT scan ya kifua chq mtu mwenye COVID-19 ikionyesha vifungu vya mwanga kwenye sehemu ya kifua

Tabia ya vipengele vya kwenye picha za radiologia yaani radiographs na en:computed tomography (CT) ya watu wenye dalili yaani symptomatic zinajumuisha asymmetric peripheral ground glass opacities na kutokuwepo kwa en:pleural effusions. Jumuia ya wanaraiologia wa kiitaliano yaani The Italian Radiological Society inafanya majumuisho ya data za kimataifa kwenye hifadhidata ya mtandaoni ya picha za kesi zilizothibitishwa. Kutokana na muingiliano wa maambukizi mengine kama adenovirus, picha bila uthibitisho wa PCR zina ukomo katika kutambua wazi COVID-19. Utafiti mkubwa uliofanyika China kulinganisha matokeo ya picha za kifua za CT na yale ya PCR yameonyesha kuwa ingawa picha hizo hazina uwezo wa kuonyesha wazi maambukizi, ni za haraka na nyeti zaidi, na kushauri kuwa pendekezo la upimaji kwenye maeneo ya maambukizi. Artificial intelligence-based convolutional neural networks zimetengenezwa kugundua vipengele vya picha ya kirusi kwa ajili ya radiologia na CT.[7]

Rejea

  1. Langlois, John P. Making a diagnosis. uk. 198. ISBN 0-306-46692-9.
  2. Langlois, John P. Making a diagnosis. uk. 204. ISBN 0-306-46692-9.
  3. Organization, World Health (2020). Laboratory testing of 2019 novel coronavirus (‎‎‎‎‎‎‎‎‎‎‎2019-nCoV)‎‎‎‎‎‎‎‎‎‎‎ in suspected human cases: interim guidance, 17 January 2020 (kwa Kiingereza). World Health Organization. ISBN 978-92-4-000097-1.
  4. CDC (2020-06-05). "Coronavirus Disease 2019 (COVID-19) in the U.S." Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-06.
  5. Brueck, Hilary. "There's only one way to know if you have the coronavirus, and it involves machines full of spit and mucus". Business Insider. Iliwekwa mnamo 2020-06-06.
  6. CDC (2020-02-11). "Information for Laboratories about Coronavirus (COVID-19)". Centers for Disease Control and Prevention (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-06-06.
  7. Li, Lin; Qin, Lixin; Xu, Zeguo; Yin, Youbing; Wang, Xin; Kong, Bin; Bai, Junjie; Lu, Yi; Fang, Zhenghan; Song, Qi; Cao, Kunlin (2020-03-19). "Artificial Intelligence Distinguishes COVID-19 from Community Acquired Pneumonia on Chest CT". Radiology: 200905. doi:10.1148/radiol.2020200905. ISSN 0033-8419. PMC 7233473. PMID 32191588.{{cite journal}}: CS1 maint: PMC format (link)