Nenda kwa yaliyomo

Nuru Inyangete : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{Mtu Mashuhuri |jina = Nuru Susan Nyerere Inyangete |picha = |caption = Nuru Susan Nyerere Inyangete |majina_mengine = |tarehe ya kuzaliwa =...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 10:15, 3 Aprili 2020

'

Nuru Susan Nyerere Inyangete
Kazi yakeMtalaamu wa usanifu majengo


Nuru Susan Nyerere Inyangete (alizaliwa 06 Desemba 1961) ni mtaalamu wa sanaa na sayansi ya Usanifu majengo [1][2]. Nuru ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya usanifu [3][4] [5]

Familia

Nuru ni moto wa mdogo wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Joseph Nyerere [6] [7]

Elimu

Nuru ana shahada ya uzamivu kwenye masomo usanifu majengo kwa msaada wa kompyuta. Pia ana shahada za sayansi na usanifu, zote alipata nchini Uingereza kati ya mwaka 1983 - 1989.

Kazi

Nuru ana uzoefu wa miaka zaidi ya 25 katika usanifu na ujenzi. Amefanya kazi nchi mbali mbali zikiwemo Uingereza, Nigeria na Tanzania. Amekua akifanya kazi kama mbunifu na mkurugenzi wa miladi mbali mbali ihusianayo na usanifu na ujenzi wa makazi, sehemu za biashara, majengo ya taasisi, usanifu wa ndani nasanifu endelevu[8][9].

Pia ametumikia kwenye bodi za taasisi mbali mbali zikiwemo bodi ya wasanifu majengo ya Tanzania (Architects and Quantity Surveyors Registration Board of Tanzania - AQRB) kama muanzilishi na mwanachama, pamoja na mamlaka ya ununuzi ya Tanzania (Public Procurement Appeals Authority of Tanzania - PPAA)[10][11].

Kazi muhimu

  • Miradi ya usanifu, ushauri wa kisanifu na ujenzi wa makazi nafuu na nyumba za jamii, miundombinu ya usafiri ya kisasa na majengo ya taasisi huko nchini Nigeria
  • Usanifu na ujenzi wa makazi ya jamii, biashara na taasisi nchini Tanzania kama vile majengo ya taasisi zikiwemo benki kuu ya Tanzania na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (National Social Security Fund) na majengo ya makazi yakiwemo makazi ya South Beach, kisota na ya shirk la nyumba Tanzania
  • Usanifu wa ofisi za shirika la kimataifa la kazi nchini Tanzania, Kenya, Somalia na Uganda
  • Zaidi ya miradi 22 ya office fit out and sehemu za burudani na starehe katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania

Tuzo

  • Medali ya fedha katika ubora wa usanifu kutoka baraza la mji wa zamani wa Strathclyde (mwanamke wa kwanza kupata medali hiyo)
  • Mshindi wa kwanza wa mradi bora wa jengo la biashara kutoka bodi ya wasanifu majengo ya Tanzania mwaka 2008
  • Mshindi wa tatu wa mradi bora kwenye eneo la maendeleo ya miundombinu ya kijamii mwaka 2011
  • Mshindi wa kwanza wa mashindano ya usanifu ya shirika la kimataifa la kazi (ILO)


Tanbihi

  1. https://www.ippmedia.com/en/business/architect-nuru-taking-her-rightful-place-profession
  2. https://www.finance-monthly.com/2018/04/real-estate-and-construction-in-africa/
  3. https://epitome-arc.com/about-us/
  4. https://www.finance-monthly.com/2018/04/real-estate-and-construction-in-africa/
  5. Folkers, Antoni S.; van Buiten, Belinda A. C. (2010). Modern Architecture in Africa: Practical Encounters with Intricate African Modernity (kwa english). The Netherlands: Springer. uk. xxii, 190, 191. ISBN 978-3-030-01074-4. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |subscription= (help)CS1 maint: unrecognized language (link)
  6. http://michuzi2.rssing.com/chan-7007653/all_p44.html
  7. http://jambotz8.blogspot.com/search?updated-max=2013-02-16T14:09:00%2B03:00&max-results=15&reverse-paginate=true&start=142&by-date=false
  8. https://www.ippmedia.com/en/business/architect-nuru-taking-her-rightful-place-profession
  9. https://www.finance-monthly.com/2018/04/real-estate-and-construction-in-africa/
  10. https://www.ippmedia.com/en/business/architect-nuru-taking-her-rightful-place-profession
  11. https://www.finance-monthly.com/2018/04/real-estate-and-construction-in-africa/