Welisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
'Cymru
Welisi (Wales)
Bendera ya Welisi Nembo ya Welisi
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Cymru am byth (Kiwelisi)
"Welisi milele"
Wimbo wa taifa: Hen Wlad Fy Nhadau (Kiwelisi)
Nchi ya mababu yangu
Lokeshen ya Welisi
Mji mkuu Cardiff
51°29′ N 3°11′ W
Mji mkubwa nchini Mji mkuu
Lugha rasmi Kiwelisi, Kiingereza
Serikali
Mfalme
Waziri Mkuu wa Ufalme
Waziri kiongozi wa Wales
Ufalme wa Kikatiba
Charles III wa Uingereza
Rishi Sunak
Mark Drakeford
Muungano wa Welisi
Mfalme Gruffudd ap Llywelyn
1056
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
20,779 km² ()
Idadi ya watu
 - 2017 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
3,124,0001 ()
3,063,456
140/km² ()
Fedha Pound sterling (GBP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
GMT (UTC0)
BST (UTC+1)
Intaneti TLD .uk2
Kodi ya simu +44

-



Ramani ya Welisi

Welisi (kutoka Kiingereza: Wales; kwa Kiwelisi: Cymru  matamshi ?: kimru) ni nchi ya Ulaya kwenye kisiwa cha Britania na sehemu ya Ufalme wa Muungano.

Welisi ni rasi kubwa inayoingia katika sehemu ya Bahari Atlantiki inayotenganisha Britania na Eire (Ireland). Inapakana na Uingereza upande wa mashariki. Pande nyingine ni pwani. Eneo lake lote lina km² 20,735.

Mji mkuu ni Cardiff (kwa Kiwelisi: Caerdydd).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Welisi ilikaliwa na makabila mbalimbali ya Kikelti wakati kisiwa cha Britania kilivamiwa na Dola la Roma katika karne ya 1 BK. Waroma walitawala hadi mnamo mwaka 400 BK.

Tangu kuingia kwa Waanglia-Saksoni kisiwani na uenezi wao katika karne ya 5 milima ya Welisi ilibaki eneo ambako utamaduni wa Wakelti uliendelea kustawi.

Kuanzia mwaka wa 1284 Welisi ilivamiwa na Uingereza na kuunganishwa kama sehemu kamili ya Ufalme wa Uingereza mwaka 1536.

Baada ya Ufalme wa Uingereza kuungana na Uskoti na Eire Welisi ilitambuliwa kama sehemu asilia ya Ufalme wa Muungano.

Katika karne ya 18 na 19 Welisi iliona kuongezeka kwa viwanda; makaa mawe na migodi ya shaba na chuma viliweka msingi wa tasnifu ya viwanda. Viwanda vya Welisi vilizalisha karibu nusu ya chuma chote cha Uingereza. Wakazi waliongezeka hasa kusini kwa sababu wafanyakazi Waingereza walihamia Welisi.

Katika karne ya 20 akiba za malighafi zilikwisha na viwanda vingi vilifungwa.

Mwaka wa 1998 Welisi ilipewa bunge lake la pekee linalosimamia matumizi ya makisio yake na kuchagua serikali ya eneo.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ni zaidi ya milioni tatu.

Lugha asilia ni Kiwelisi ambacho ni kimoja kati ya lugha za Kikelti. Leo hii kuna bado asilimia 19 za wakazi wanaotumia Kiwelisi lakini wengine wamezoea zaidi Kiingereza. Wasemaji wa Kiwelisi wako hasa kaskazini na kwenye sehemu ya milima ambako kuna maeneo ambako idadi kubwa ya watu huongea lugha hii wakijua Kiingereza kama lugha ya pili.

Upande wa dini, 57.6% ni Wakristo, hasa Waanglikana. 0.8% ni Waislamu. 32.1% hawana dini yoyote.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Welisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.