Petro wa Moutiers

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Petro wa Moutiers, O.Cist. (Saint-Maurice-de-l'Exil, 1102 - Bellevaux, 14 Septemba 1174) alikuwa askofu wa mji huo, leo nchini Ufaransa[1].

Baada ya kukariri Zaburi zote, akiwa na umri wa miaka 20 alijiunga na monasteri ya Wasitoo. Hata wazazi wake na ndugu zake watatu wakawa wamonaki[2].

Miaka 10 baadaye alifanywa abati wa monasteri mpya[3], na miaka 10 tena baadaye askofu kwa pendekezo la Bernardo wa Clairvaux.

Aliongoza vizuri ajabu jimbo lake akilitembelea lote, akisaidia maskini[4] na kumpinga kaisari Frederick I Barbarossa aliyemsimamisha antipapa Vikta IV dhidi ya Papa Aleksanda III. Pia aliteuliwa kupatanisha wafalme.

Papa Selestini III alimtangaza mtakatifu mwaka 1191.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92372
  2. Saint Peter of Tarentaise. Saints SQPN (19 September 2017). Retrieved on 1 October 2017.
  3. "St. Peter of Tarentaise, Bishop", Catholic Exchange
  4. ""Saint Peter of Tarentaise", Franciscan Media". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-08. Iliwekwa mnamo 2020-09-13.
  5. Martyrologium Romanum

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. London:Penguin Books, 3rd edition, 1995. ISBN|0-14-051312-4.
  • Rabenstein, Katherine (Agosti 1999). "Peter of Tarentaise, OSB Cist. B." Saints O' the Day for May 8. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 2012-02-23.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unfit URL (link)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.