Nenda kwa yaliyomo

Nyakonga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Nyakonga
Kata ya Nyakonga
Wilaya ya Tarime ilipo
Wilaya ya Tarime ilipo
Wilaya ya Tarime ilipo
Nyakonga is located in Tanzania
Nyakonga
Nyakonga

Mahali pa Nyakonga

Majiranukta: 1°21′03″S 34°34′17″E / 1.3507°S 34.5715°E / -1.3507; 34.5715
Nchi Tanzania
Mkoa Mkoa wa Mara
Wilaya Wilaya ya Tarime
Kata Nyakonga
Vijiji 3
Serikali
 - Diwani Simon Kiles Samwel
 - Mtendaji Kata
Idadi ya wakazi (Sensa 2022)
 - Wakazi kwa ujumla 9,215
EAT (UTC+3)
Msimbo wa posta 31415 [1]
Tovuti:  tarimedc.go.tz

Nyakonga ni kata ya Wilaya ya Tarime katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31415.[1]

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 9,215 [2]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,797 waishio humo.[3]

Ofisi ya kata inapatikana katika kijiji cha Magoto.

Vijiji vya kata ya Nyakonga[hariri | hariri chanzo]

Kata hii ina vijiji 3 na vitongoji 12.[1]

  • Magoto
    • Nyanswega Nyangwe Gakendo
    • Nyangwe
    • Gakendo
  • Nyakonga
    • Komomendi
    • Buchora
    • Komagori
    • Kebweye
    • Senta
    • Nyang'iti
  • Kebweye
    • Nyakonga
    • Mkuyuni
    • Nyamesanga
    • Keburwi

Huduma za jamii[hariri | hariri chanzo]

Huduma za afya katika kata ya Nyakonga zinapatikana katika kijiji cha Magoto ambapo kuna kituo cha afya[4] na katika kijiji cha Kebweye ambapo kuna zahanati.

Huduma za elimu ya awali na msingi zinapatikana katika vijiji vyote vitatu, ambapo kuna shule za awali za serikali na za binafsi na shule za msingi za serikali. Kwa upande wa elimu ya sekondari kuna shule ya sekondari Magoto[5] ambayo inapatikana katika kijiji cha Magoto. Shule hiyo inatoa elimu kuanzia darasa la 9 (kidato cha kwanza) mpaka darasa la 14 (kidato cha sita).[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 https://www.tcra.go.tz/uploads/text-editor/files/Mara%2031000_1622732858.pdf
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 190
  3. Sensa ya 2012, Mara - Tarime-District-Council
  4. "Magoto Health Center". Doctor 4 Africa (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-02-21.
  5. "Magoto Secondary School Mara | Education | Tanzania | SaaHiiHii". www.saahiihii.com. Iliwekwa mnamo 2024-02-21.
  6. "Magoto Secondary School Profile | Angazetu" (kwa American English). 2024-02-09. Iliwekwa mnamo 2024-02-21.
Kata za Wilaya ya Tarime Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania

Binagi * Bumera * Ganyange * Gorong'a * Gwitiryo * Itiryo * Kemambo * Kibasuka * Kiore * Komaswa * Kwihancha * Manga * Matongo * Mbogi * Muriba * Mwema * Nyakonga * Nyamwaga * Nyansincha * Nyanungu * Nyarero * Nyarokoba * Pemba * Regicheri * Sirari * Susuni


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyakonga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.