Lomasontfo Dludlu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lomasontfo Martha Dludlu (amefariki 10 Januari 2011) alikuwa mwanasiasa wa Eswatini. Mwaka 1993 alikuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika Bunge la nchi hiyo.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Dludlu alikulia katika eneo la vijijini ambapo hakupata elimu rasmi.[1] Alifanya kazi kama mhamasishaji wa jamii na alihudumia wakazi wenye ulemavu na mayatima.[1]

Licha ya kutokuwa na elimu, aligombea Uchaguzi Mkuu wa Eswatini mwaka 1993 huko Maphalaleni na kuchaguliwa katika Baraza la Wawakilishi, akishinda wanaume nane na mwanamke mmoja, na kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa katika Baraza hilo.[1] Aliendelea kuwa mwanachama hadi Uchaguzi Mkuu wa Eswatini mwaka 1998.[1]

Aliugua kiharusi mwaka 2008 akafariki nyumbani kwake tarehe 10 Januari 2011 akiwa na umri wa miaka 64.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Toolkit for Gender Sensitive Electoral Education Women and Law Southern Africa
  2. First woman MP passes on Times of Swaziland, 13 January 2011
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lomasontfo Dludlu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.