Kasumba ya tikitimaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanzoni mwa karne ya 20, kadi kadhaa za posta zilitengenezwa kuonesha kasumba ya tikitimaji; hii ni moja wapo.

Kasumba ya tikitikimaji ni mtazamo wa kikasumba ambao watu weupe wa Marekani] wa wakati huo walikuwa wanaamini ya kwamba watu weusi wanaweza kufurahishwa kiubwete kabisa; wanahitaji tikitimaji na mapumziko kidogo basi hiyo ni furaha yao tosha kabisa.[1] Kasumba ilidumisha kiasi kwamba Wamarekani Weusi walikuwa wanachukuliwa kama mabwege na mafala tu katika jamii yao na wapenda kazi bure, wakawatungia hadi wimbo wakati huo kwa kupenda tikitimaji.[2] Kasumba hii Marekani ndiyo inatamba sana, na inarudi tangu zama zile za utumwa, watu ambao walikuwa wanaendekeza biashara ya utumwa walionesha ya kwamba watu weusi walikuwa watu wenye akili za kawaida na wanahitaji vitu vichache tu ili wawe na furaha.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Wade, Lisa. "Watermelon: Symbolizing the Supposed Simplicity of Slaves". Iliwekwa mnamo Machi 30, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Fences: Shmoop Literature Guide. 2010. uk. 26. ISBN 9781610624190. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-10-19. Iliwekwa mnamo 2017-09-06. {{cite book}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)