Joakima wa Vedruna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Joakima mwaka 1903.

Joakima wa Vedruna (jina kamili kwa Kikatalunyaː Joaquima de Vedruna Vidal de Mas; Vic, Barcelona, Hispania, 17 Aprili 1783 - Sevilla, 28 Agosti 1854) alikuwa sista mwanzilishi wa shirika la Masista Wakarmeli wa Upendo ambalo ndani ya Kanisa Katoliki linahudumia vijana, wagonjwa na wazee waliosahaulika. Kwa sasa lina masista 2,000 hivi duniani kote[1].

Kabla ya hapo aliishi katika ndoa akazaa watoto tisa aliowalea Kikristo sana [2][3], lakini baada ya kufiwa mumewe alianzisha shirika hilo kwa kuvumilia aina nyingi za matatizo hadi alipofariki dunia kwa kipindupindu[4].

Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 19 Mei 1940, halafu Papa Yohane XXIII alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Aprili 1959.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[5].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Saint Joaquina Vedruna Vidal de Mas". Saints SQPN. 11 Juni 2015. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "St. Joaquina de Vedruna". Spread Jesus. 16 Oktoba 2011. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Joachima de Vedruna de Mas (1783-1854)" (PDF). CarmelNet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2021-08-23. Iliwekwa mnamo 12 Januari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. http://www.santiebeati.it/dettaglio/67875 Santi e Beati
  5. Martyrologium Romanum

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Itúrbide, Emilio: Del matrimonio a la gloria de Bernini: Santa Joaquina Vedruna, fundadora del Instituto de Hermanas Carmelitas de la Caridad. Ejemplo vivo para todos los estados de la vida, Pamplona: Gómez, 1959

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.