Iraq

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
جمهورية العراق
Jumhūrīyat al-`Irāq
كۆماری عێراق
Komara `Îraqê

Jamhuri ya Iraq
Bendera ya Iraq Nembo ya Iraq
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kiarabu: الله أكبر
(Allahu Akbar)
(Translation: "Mungu ni mkuu")
Wimbo wa taifa: Mawtini (new);
Ardh Alforatain (previous)[1]
Lokeshen ya Iraq
Mji mkuu Baghdad[2]
33°20′ N 44°26′ E
Mji mkubwa nchini Baghdad
Lugha rasmi Kiarabu, Kikurdi[3]
Serikali Jamhuri, serikali ya kibunge
Barham Salih
Mustafa Al-Kadhimi
Uhuru
kutoka Dola la Uturuki
kutoka Uingereza

31 Oktoba 1919
3 Oktoba 1932
28 Juni 2004
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
437,072 km² (ya 59)
1.1
Idadi ya watu
 - 2015 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
37,056,169 (ya 36)
82.7/km² (ya 125)
Fedha Iraqi Dinar (IQD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC+4)
Intaneti TLD .iq
Kodi ya simu +964

-

1 Wakurdi hutumiaEy Reqîb.
2 Arbil ni mju mkuu wa jimbo la kujitawala la Kurdistan.
3 Lugha rasmi za serikali kitaifa ni Kiarabu na Kikurdi. Kikurdi ni lugha rasmi ya jimbo la Kurdistan. Kikatiba lugha za Kiassiryani na Kiturkmeni ni lugha rasmi kieneo penye wasemaji wengi wa lugha hizi.


Ramani ya Iraq

Iraq (kwa Kiarabu العراق, al-ʿIrāq) ni nchi ya Asia ya Magharibi inayokaliwa hasa na Waarabu (75-80%) lakini pia na wengine, hasa Wakurdi 15%).

Inajumlisha eneo la Mesopotamia pamoja na sehemu ya jangwa la Shamu na ya milima ya Zagros.

Imepakana na Kuwait, Saudia, Yordani, Syria, Uturuki na Uajemi. Kuna pwani fupi kwenye Ghuba ya Uajemi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya Iraq ni jangwa lakini kuna eneo lenye rutuba kati ya mito ya Frati na Hidekeli.

Kaskazini ni hasa nchi ya milima inayopanda hadi ya kimo cha m 3,611 juu ya UB.

Hali ya hewa inalingana na mazingira. Kipindi cha kiangazi kuna joto kali. Majira ya Desemba-Februari kuna halijoto ya kupoa kusini na baridi kali mlimani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Iraq ni nchi yenye historia ndefuː ilikuwa kitovu cha ustaarabu wa binadamu, mahali pa miji ya kwanza duniani katika Sumeri na Babeli.

Baada ya kusambaratika kwa milki ya Waturuki Waosmani walioitawala muda mrefu, Iraq ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa nchi lindwa chini ya athira ya Uingereza hadi mwaka 1958.

Miaka ya hivi karibuni imejulikana hasa kutokana na vita mbalimbaliː kwanza vita dhidi ya Uajemi chini ya serikali ya Saddam Hussein tangu 1981, baadaye vita dhidi ya Kuwait na Marekani.

Vita vya pili vya ghuba ya 2003 iliyoleta uvamizi wa Marekani ilizidi kuleta vifo na uharibifu.

Hatimaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoingiliwa na DAESH iliyoteka sehemu kubwa ya nchi, hasa kaskazini na magharibi, hadi mwishoni mwa mwaka 2017.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Lugha rasmi na ya kwanza ni Kiarabu, ikifuatwa na Kikurdi ambayo pia imekuwa lugha rasmi, halafu lugha nyingine za jamii mbalimbali ambazo pengine zinatambulika kieneo.

Wakazi wengi (95%), hasa baada ya vita vya hivi karibuni, ni Waislamu, wakiwemo kwanza Washia halafu na Wasuni. Wakristo waliobaki ni 5%, wakiwemo hasa waamini wa Kanisa Katoliki la Wakaldayo na Waashuru wa Kanisa la Mashariki.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Iraq ina akiba kubwa za mafuta ya petroli ardhini. Mapato kutokana na mafuta yalileta maendeleo makubwa nchini hadi mwanzo wa kipindi cha vita vilivyoharibu sana nchi pamoja na uchumi wake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Taarifa za jumla
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iraq kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.