Florentina wa Cartagena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake.

Florentina wa Cartagena (Cartagena, leo nchini Hispania, 545/550 - labda Sevilia, Hispania, 612 hivi) alikuwa bikira ambaye aliongoza monasteri mbalimbali kufuatana na kanuni aliyopewa na kaka yake Leandri wa Sevilia kwa jina la De institutione virginum et contemptu mundi [1].

Alizaliwa na Severianus na Turtura akiwa mmoja kati ya watoto watano, ambao kati yao watatu wengine wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu: Leandri, Fuljensi na Isidori wa Sevilia, wote maaskofu[2].

Mwanamke mwenye elimu, aliandikiwa na kaka zake vitabu mbalimbali [3][4].

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Agosti[5].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Patrologia Latina, LXXII, 873 n.k.
  2. "Saint Florentina of Cartagena". Saints.SQPN.com. Iliwekwa mnamo 2012-07-16.
  3. http://www.santiebeati.it/dettaglio/67830
  4. St. Florentina - Saints & Angels - Catholic Online
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.