Emiliani wa Silistra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro mdogo wa Mt. Emiliani.

Emiliani wa Silistra (alifariki Silistra, Mesia, leo nchini Bulgaria, 18 Julai 362) alikuwa kijana wa Durostoro aliyeuawa kwa ajili ya imani ya Kikristo katika dhuluma ya Juliani Mwasi. Akikataa kutii amri ya kaisari huyo, na vitisho vya mwakilishi wake Catulinus, alipindua altare ya miungu ili kuzuia isitolewe sadaka. Ndipo alipotupwa katika tanuru akafa kwa kuungua moto [1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 18 Julai[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/93035
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.