Bugongi, Kabale, Uganda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Uganda


Majiranukta: 01°14′44″S 29°59′17″E / 1.24556°S 29.98806°E / -1.24556; 29.98806
Country Uganda
Region Western Uganda
Sub-region Kigezi sub-region
District Kabale District
City Kabale
Serikali
 - Division Chairman Isaac Mucunguzi Rushoga[1]
Mwinuko  5,935 ft (1,810.2 m)
Idadi ya wakazi (2014 Census)
 - Wakazi kwa ujumla 36,000[1]

Bugongi ni mji uliopo jirani na mji wa Kabale, ndiyo sehemu kubwa katika mji na makao makuu ya wilaya ya Kabale nchini Uganda.[1]

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Bugongi ipo upande wa kaskazini mwa mji wa Kabale, takribani kilomita 2 kaskazini mwa mji mkuu wa kibiashara katika wilaya hiyo.[2] Majira nukta ya kijiografia ya Bugongi ni: 01°14'44.0"S, 29°59'17.0"E (Latitude:-1.245556; Longitude:29.988056).

Kata ya mwisho ya Bugongi ipo kwenye mwinuko wa wasta wa mita 1809, kutoka usawa wa Bahari.[3]

Idadi ya watu[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2012, ofisi ya takwimu ya Uganda ilikadiria idadi ya watu wa Bugongi kuwa ni 25,000.[1] Sensa ya taifa ya watu na makazi ya mwaka 2014 ilionesha idadi ya watu imefikia 36,000.[1]

Hapo nyuma, mnamo mwaka 2005 ama kabla ya hapo, Bugongi ilikuwa na sifa mbaya kama makazi duni, yanayochochea vitendo vya wizi, ukahaba, na uvutaji bangia.[1] Hivyo, tangu wakati huo, makazi mapya na ya kisasa yamekuwa yakijengwa, idadi ya makanisa imeongezeka na taasisi mpya za elimu za jirani zimekuwa zikiwavutia wanafunzi na kuwaongezea hadhi na viwango vya maisha.[1] Eneo la jirani limeunganishwa na gridi ya taifa ya umeme na linahudumiwa na shirika la taifa la maji safi na maji taka.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 Sarah Asiimwe, and Robert Muhereza (8 Agosti 2018). "Bugongi, Kabale's Biggest Student Hub". Daily Monitor. Kampala. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Globefeed.com (8 Agosti 2018). "Distance between Skyline Hotel, Kabale-Kisoro Road, Kabale, Uganda and Bugongi, Kabale, Uganda". Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Mapcarta (8 Agosti 2018). "Elevation of Lower Bugongi Ward, Kabale, Uganda". Mapcarta.com. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)