Ben Pol

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ben Pol
Jina la kuzaliwaBenard Michael Paul Mnyang’anga
Pia anajulikana kamaBen Pol
Amezaliwa8 Septemba 1989 (1989-09-08) (umri 34)
Dar es salaam
Kazi yakeMwimbaji
Mwigizaji
AlaSauti
Miaka ya kazi2009-hadi sasa
Ameshirikiana naDarassa, Saida Karoli, Belle 9

Benard Michael Paul Mnyang’anga (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ben Pol; amezaliwa 8 Septemba 1989) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji kutoka nchini Tanzania. Hasa anaimba muziki wa R&B.

Ben Pol alianza kuvuma mwaka 2010 baada ya kutoa kibao cha "Nikikupata" ambacho kiliweza kumtambulisha katika ulimwengu wa Bongo Flava. Baadaye akaja kutamba zaidi na vibao kama vile Samboira, Moyo Mashine, Jikubali, Namba One Fan, TATU, Sophia n.k.

Kwa asili Ben ni mtu wa Dodoma[1], tena anajisifu kama mtu kutoka kanda ya kati.

Upande wa filamu, amepata kucheza katika filamu ya Sunshine na baadhi tu ya filamu zilizokuwa chini ya MFDI Tanzania na kuongozwa na Karabani.[2]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. [1]Archived 19 Mei 2014 at the Wayback Machine. katika Bongo Swaggz
  2. Sunshine "Ben Pol akicheza kama m-bwia unga".
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ben Pol kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.