Atanasi wa Napoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa ukutani ukiwaonyesha Wat. Atanasi na Januari.

Atanasi wa Napoli (Napoli, 832 hivi - Veroli, Frosinone, 872) alikuwa askofu wa Napoli, Italia Kusini, kuanzia mwaka 849 anayesifiwa kwa uadilifu wake na kwa juhudi za kurekebisha wakleri wa jimbo lake[1].

Baada ya mtoto wa ndugu yake kumtesa sana[2], alifukuzwa jimboni[3][4][5].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Julai[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.