Amir H. Jamal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Amir Habib Jamal (26 Januari 1922 - 21 Machi 1995) alikuwa mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Tanzania ambaye aliwahi kuwa waziri enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.[1][2] Aliwakilisha jimbo la Morogoro kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1985.[3] na alikuwa Waziri wa fedha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi kwani aliongoza wizara hiyo kwa takriban miaka 12.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Jamal alizaliwa na Wahindi walioishi Tanganyika, ambayo ni Tanzania leo.[4]. Alikuwa mtoto wa Kulsum Thawer na Habib Jamal, mwanachama mwanzilishi wa Chama cha Waasia. Alisoma katika mji wa Mwanza na akaenda kusoma elimu yake ya sekondari katika jiji la [Dar es Salaam]]. Alihitimu masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Calcutta nchini India katika fani ya uchumi bcom.[1]

Alikuwa na ndoto ya kufundisha kama daktari katika Chuo Kikuu cha Mumbay Lakini licha ya alama zake za juu, hakuingia katika kitivo cha matibabu.[5]. Mwaka 1942, Alihudhuria mkutano wa Bunge la Kitaifa la India ambapo Mahatma Gandhi alizindua harakati za kuiacha india, akidai uondoaji wa haraka wa Dola la Uingereza nchini India.[6] Baada ya kuhitimu, alirudi Dar es Salaam na kujiunga na biashara ya familia.[5]

Alikutana mara ya kwanza na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1952 katika mapokezi ya Baraza la Uingereza kwa heshima ya kurudi baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.[7] Alikuwa mzee wa harakati za uhuru wa Tanganyika, na mwaka wa 1955 alisaidia kulipa bili ya ziara ya Nyerere kwenda [[Umoja wa Mataifa] huko katika jiji la New York marekani.[8]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Europa Publications (2003). The International Who's Who 2004. Psychology Press. ku. 804–. ISBN 978-1-85743-217-6.
  2. "Biography: Amir H. Jamal". Centre for Global Negotiations. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-25. Iliwekwa mnamo 3 Machi 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Amir Habib Jamal: A Tribute from Mwalimu J.K. Nyerere" (PDF). Dag Hammarskjöld Foundation. 1995. uk. 95. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2015-07-25. Iliwekwa mnamo 25 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Godfrey Mwakikagile (2006). Life Under Nyerere. Intercontinental Books. ku. 95–. ISBN 978-0-9802587-2-1.
  5. 5.0 5.1 Judith Márffy-Mantuano Hare Countess of Listowel (1965). The Making of Tanganyika. Chatto & Windus.
  6. Vassanji 2014, p. 327
  7. Colin Legum; G. R. V. Mmari (1 Januari 1995). Mwalimu: The Influence of Nyerere. James Currey Publishers. ku. 7–. ISBN 978-0-85255-386-2.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Ronald Aminzade (31 Oktoba 2013). Race, Nation, and Citizenship in Post-Colonial Africa: The Case of Tanzania. Cambridge University Press. ku. 108–. ISBN 978-1-107-04438-8.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)