Amato wa Habend

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Amato ya karne ya 17.

Amato wa Habend (Grenoble, leo nchini Ufaransa, 565 hivi - 13 Septemba 628 hivi) alikuwa mmonaki padri maarufu kwa ugumu wa maisha, saumu na hamu ya upweke.

Pamoja na Romariki alianzisha monasteri dabo kwenye mlima Habend akaiongoza kwa busara lakini, kabla na baada ya hapo, aliishi miaka kadhaa kwa toba kali upwekeni [1].

Alitangazwa na Papa Leo IX kuwa mtakatifu mwaka 1049 pamoja na wafuasi wake Romariki na Adelfo wa Remiremont.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • (Kijerumani) Biographisch-Bibliographisches Kirchenlexikon
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.