Alkibiades

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alkibiades akifundishwa na Sokrates (taswira ya François-André Vincent (1746–1816))

Alkibiades, mwana wa Kleinias (Ἀλκιβιάδης, mnamo 450 KK - 404 KK) alikuwa mwanasiasa, mhutubu na mwanajeshi mashuhuri kutoka mjini Athini katika Ugiriki ya Kale. Alikuwa na majukumu muhimu wakati wa Vita ya Peloponesi kati ya Sparta na Athini.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika familia tajiri. Mwanafalsafa Sokrates alikuwa mwalimu wake.[1]

Wakati wa vita ya Peloponesi Alkibiades alibadilisha utii wake wa kisiasa mara kadhaa. Kwake nyumbani Atheni alipigania sera za kigeni Zza kushambulia pamoja na kampeni dhidi ya miji ya Sisilia mnamo 415 KK. Alipokosolewa na kushtakiwa baada ya kampeni hiyo akakimbilia Sparta alipokuwa mshauri wa maadui wa Athini. Baada ya kupata maadui Sparta pia aliendelea kukimbia hadi Milki ya Uajemi. Baadaye marafiki zake wa Athini waliomba arudi, hivyo akarudi akaongoza tena jeshi la Athini katika mapigano dhidi ya Sparta.

Baada ya kushinda, wapinzani waliogopa atapata mamlaka kubwa mno akaamriwa kuondoka mjini Athini. Alikimbilia tena Milki ya Uajemi. Huko aliuawa mwaka 404 KK na askari Waajemi, wengine wanasema kufuatana na maombi ya viongozi wa Sparta.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

    • "Alcibiades was an Athenian general in the Peloponnesian War". Bingley. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-02-12. Iliwekwa mnamo 2021-03-10.
    • "Alcibiades". Endres, Nikolai. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Septemba 2006. Iliwekwa mnamo 22 Septemba 2006. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
    • "Alcibiades: Aristocratic Ideal or Antisocial Personality Disorder". Evans, Kathleen. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Agosti 2006. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2006. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
    • "Alcibiades". Meiggs, Russell. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
    • "Alcibiades". Prins, Marco-Lendering, Jona. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 31 Agosti 2006. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2006. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
    • "Alcibiades". The Columbia Encyclopedia, Sixth Edition. 2001–05. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-22. Iliwekwa mnamo 5 Agosti 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)