Abebe Bikila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Abebe Bikila

Abebe Bikila (7 Agosti 1932 - 25 Oktoba 1973) alikuwa mwanariadha wa Ethiopia ambaye aliwahi kupata medali mbili za dhahabu katika za mbio za masafa marefu katika mashindano ya Olimpiki na kuwa Mwafrika wa kwanza kupata medali katika mashindano ya Olimpiki.

Zaidi ya kuwa mwanariadha, Abebe alifanya kazi katika jeshi la walinzi wa Mfalme Haile Selassie.

Rekodi[hariri | hariri chanzo]

Abebe Bikila alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki ya Roma, Italia mwaka 1960. Ushindi huo ulimpa heshima kubwa ya kitaifa. Katika mashindano hayo aliweka rekodi ya dunia ya mbio za marathoni ya masaa 2 na dakika 15 na sekunde 16.2. Abebe alishinda mbio hizo ingawa alikimbia miguu mitupu.

Medali ya pili ya dhahabu aliipata mwaka 1964 huko Tokyo, Japani. Katika mbio hizo Abebe alivaa viatu. Kilichoshangaza wengi ni kuwa wiki sita kabla ya mashindano hayo, Abebe alikuwa na operesheni ya kuondoa kibole. Operesheni hiyo ilimzuia kufanya mazoezi ya kujiandaa kwa mbio hizo. Hata hivyo aliweza kushiriki na kushinda. Baada ya kumaliza mbio hizo, Abebe Bikila alishangaza watazamaji kwa kuendelea kukimbia na kufanya mazoezi mengine. Wakimbiaji wengine waliishiwa nguvu kabisa baada ya kumaliza kukimbia na hata kufikia hatua ya kuzimia.

Katika mashindano ya Tokyo, Abebe aliweza kuvunja rekodi yake mwenyewe kwa kukimbia kwa masaa 2, dakika 12 na sekunde 11.2.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Abebe Bikila alifariki kwa kuvuja damu kwenye ubongo kutokana na ajali ya gari. Ajali hiyo ilikuwa mbaya kiasi cha kupooza mwili wake toka kiunoni kwenda chini.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Abebe Bikila kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.