Zangalewa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Zangalewa (Zamina mina, kwa jina lingine) ni wimbo uliorekodiwa mwaka wa 1986 na kikundi cha densi cha Zangalewa (Bendi la Muziki). Wimbo huu unajulikana nchi karibu zote za Afrika, na kutumiwa na skauti, polisi na wanajeshi wa nchi hizo haswa katika mazoezi yao. Umeimbwa katika lugha kadhaa zinazopatikana nchi za Afrika Magharibi.

Katika lugha ya Kiduala, maana ya "Zangalewa?" ni "Nani alikuita?", ama, "Nani alikuambia uingie kwenye jeshi?"

Chanzo[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Vita Kuu ya Dunia, nchi ya Ufaransa ilitumia watawala wake kutoka nchi ya [Kamerun] kusababisha vijita na ugomvi katika kambi za adui kabla ya jeshi lao kuu (la Ufaransa) kupigana na adui. Mkameruni aliyekuwa amejisajili kuingia jeshi hilo basi alijiambia kwa huzuni, "edjibe zangalewa!" Neno "edjibe" ni neno faragha linaloweza kuonyesha hisia tofauti kama hasira, furaha, mshangao, nk. Kwa Kiswahili, njia moja ya kusema "Edjibe zangalewa!" ni, "Daa! Nini kilichokuleta hapa?!"

Maana[hariri | hariri chanzo]

Emeli Kojidie, kiongozi wa bendi la Zangalewa anasema kuwa[1] wimbo huo unaweza kuwa na maana mbili:

  1. Kuwakejeli wenzao, haswa Askari Kanga na machifu, waliosaidia mabeberu kuwahujumu.
  2. Kuwasifu wanajeshi hao jasiri kwa kupigana katika vita hivyo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]