Valdo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Petro Valdo, Worms, Ujerumani.

Petro Valdo (kwa Kifaransa: Pierre Vaudès/de Vaux, 1140 hivi - 1179 au 1205 hivi), anatajwa kwa mwanzilishi wa Wavaldo, tapo la Ukristo la Karne za Kati.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Hakuna habari nyingi za hakika kuhusu maisha yake. Mfanyabiashara wa Lyon, Ufaransa, aliongoka kwa kuacha mali yake na kushika ufukara[1][2][3].

Alianza pia kuhubiri, hasa kwamba, "Hakuna anayeweza kuyumikia mabwana wawili, Mungu na mali".[4] Kufikia mwaka 1170 Valdo alikuwa ameshapata wafuasi wengi walioiga maisha yake ya Kiinjili.[5]

Anasifiwa pia kwa kutoa au kuagiza tafsiri ya kwanza ya Biblia katika lugha yoyote mpya iliyotokana na Kilatini.[6]

Mwaka 1179, Valdo na mfuasi wake mmojawapo walikwenda Roma, walipokaribishwa na Papa Alexander III. Mwaka huohuo mtaguso wa tatu wa Laterano ulikataa baadhi ya mawazo ya Valdo, bila kulaani tapo lenyewe wala kutenga viongozi wake.

Lakini itikio la maaskofu lilikuwa kali zaidi, hivyo Wavaldo walifukuzwa kutoka Lyon, na hatimaye walijitafutia usalama katika mabonde ya Piemonte, Italia Kaskazini.[7]

Baada ya mwanzo wa Matengenezo ya Kiprotestanti, Wavaldo walijiunga nayo, hasa katika mfumo wa Wakalvini (1532).[8]

Kwa sasa Wavaldo ni 70,000 hivi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Jean Paul Perrin, History of the Old Waldenses Anterior to the Reformation, (New York: 1884) pg 21
  2. Jones, vol 2, pg 8
  3. M. Aston, Faith and Fire: Popular and Unpopular Religion, 1350-1600, (London, 1993) p.18.
  4. Perrin, pg 22
  5. JA Wylie, History of the Waldenses, (London: 1848), pg 17
  6. Jones, vol 2, pg 10
  7. [1]
  8. Ellwood, Robert S. and Gregory D. Alles, eds. (2007) The Encyclopedia of World Religions, p. 471. Infobase Publishing, New York

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Audisio, Gabriel, The Waldensian Dissent: Persecution and Survival, c.1170 - c.1570, Cambridge Medieval Textbooks. (1999) Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 0-521-55984-7

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.