Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1892

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1892 ulikuwa wa 27 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 8 Novemba. Upande wa "Democratic Party", Rais Grover Cleveland (pamoja na kaimu wake Adlai Stevenson) aliwashinda mgombea wa "Republican Party" Rais Benjamin Harrison (pamoja na kaimu wake Whitelaw Reid) na mgombea wa "Populist Party" James B. Weaver (pamoja na kaimu wake James G. Field).

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Cleveland akapata kura 277, Harrison 145 na Weaver 22. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.