Lobamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Lobamba
Nchi Eswatini
Mahali pa Lobamba nchini Eswatini.

Lobamba ni kati ya miji mikuu miwili ya Eswatini. Lobamba ni mji mkuu wa mfalme na pia makao ya bunge la nchi. Serikali inakaa Mbabane.

Lobamba inaona sherehe kubwa ya kitaifa kila mwaka ni ngoma ya Umhlanga au ngoma ya mafunjo ambako wasichana wanachukuwa mafunzo na kuzipeleka kwa ikulu ya ntombi (mama wa mfalme). Ni kawaida ya kwamba mfalme anaweza kumteua mke mpya kati ya wasichana hawa wakicheza.

Majengo maalumu ni pamoja na ikulu, boma la kifalme, jumba la mama wa mfalme, Makumbusho wa Kitaifa ya Uswazi, Bunge na makumbusho ya mfalme Sobhuza II.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lobamba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.