Fuwawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa fuwawe kutoka volkeno ya Teide kwenye kisiwa cha Tenerife, Visiwa vya Kanari. Densiti yake ni takriban 0.25 g/cm³. Skeli inaonyesha sentimita.
Picha ya fuwawe inaonyesha uwingi wa mashimo na nafasi ndani yake

Fuwawe (pia: fuwe; ing. pumice) ni aina ya mwamba mwepesi inayoundwa na povu ya zaha (lava).

Maana yake zaha ambayo ni mwamba joto sana katika hali ya kiowevu inarushwa kutoka volkeno kwa shinikizo kubwa inakuwa kama povu kwa sababu shinikizo inapungua haraka sana. Ikipoa haraka umbo hili linaganda kuwa thabiti na kubaki vile.

Kwa hiyo asili ya fuwawe ni daima mlipuko wa volkeno.

Fuwawe inatokea kama mkusanyiko wa vipande-vipande au pia kama maganda manene.

Mara nyingi ni nyepesi kiasi inaelea juu ya maji, angalau kwa muda hadi maji yanaingia na kujaza polepole nafasi ndani yake.

Kiasili inatumiwa kwa kusugua na kusafisha ngozi. Fuwawe iliyosagwa inatumiwa pia kwa kusafisha meno kwa msaada wa mswaki.

Kuna pia matumizi ya fuwawe kwa ujenzi maanake ni kifaa chepesi chenye tabia nzuri za kuhami dhidi ya baridi na joto. Kwa kawaida inapondwa, kuchanganywa na kiasi kidogo cha saruji[1] lakini kuna pia majaribio ya kuitumia vile.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. When technology fails - Pumice Crete, uk. 161, via google books, ilitazamiwa Juni 2016
  2. Building with pumice

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: