Mfalme Yehu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"Yehu mwana wa Omri" akitoa heshima yake kwa mfalme mkuu wa Ashuru: Black Obelisk ya Shalmaneser III.

Mfalme Yehu (kwa Kiebrania יֵהוּא, Yēhû, maana yake: "YHWH ni mwenyewe"[1] ) alikuwa mfalme wa kumi wa Israeli baada ya Yeroboamu I.

Ni maarufu kwa kuangamiza ukoo wa Ahabu ili kuokoa imani ya Mungu pekee iliyokaribia kutoweka kwa juhudi za malkia Jezebeli. Hivyo alikamilisha kazi ya manabii Elia na Elisha.

Hata hivyo Biblia inamlaumu kama waandamizi wote wa Yeroboamu I kwa kuvumilia mahekalu mbadala ya Betel na Dan.

Alikuwa mwana wa Yehoshafati,[2] na mjukuu wa Nimshi.

William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu miaka 842815 KK, wakati E. R. Thiele alikadiria miaka 841814 KK.[3]

Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha pili cha Wafalme, sura 9-10.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Meaning of Jehu - History and Origin Archived 21 Machi 2012 at the Wayback Machine. – Meaning of "Jehu", Hebrew name, Meaning-of-Names.com.
  2. Jehu's father was not the roughly contemporaneous King Jehoshaphat of Judah, whose own father was King Asa of Judah. "Generally Jehu is described as the son only of Nimshi, possibly because Nimshi was more prominent or to avoid confusing him with the King of Judah (R’Wolf)". Scherman, Nosson, ed., "I–II Kings", The Prophets, 297, 2006. See (2 Kings 9:2)
  3. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Yehu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.