Abbasizo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Abbas Ally Mlyuka (pia Abbasizo; amezaliwa 1981 katika mji wa Iringa nchini Tanzania) ni mtangazaji katika redio, pia ni mwandishi wa habari.

Amesoma katika shule ya msingi Gangilonga, amesoma sekondari za Mwembetogwa na Highland , zote za mjini Iringa.

Amesoma uhandisi wa sauti na utayarishaji wa muziki katika chuo cha emende.

Abbas ni mtoto wa mkulima Ally Mlyuka ambae ni maarufu katika kilimo cha mahindi katika jimbo la Ismani (wilaya ya Iringa vijijini). Ni mtoto wa mwisho kwa mama yake kati ya watoto saba.

Abbas akiwa rafiki yake Frank Ugumba ndio wasanii wa kwanza kurekodi katika cd muziki wa kizazi kipya mkoani Ruvuma.

Abbasizo ni jina lake la kazi alilolipata alipokuwa mtangazaji wa radio songea ambapo pia ni kati wa waanzilishi wa kituo hicho cha radio mkoani ruvuma kinachomilikiwa na halmashauri ya songea. Abbas na rafiki yake Kilian Francis ndunguru ndio wanzilishi wa kwanza wa studio ya muziki mkoani ruvuma sosizo record na mmiliki wa studio ya sosizo record ya mkoani iringa 2003.

Akiwa mdogo wa umri wa miaka sita alipenda muziki ambapo huko nyumbani kwao iringa mjini kata ya makorongoni mtaa wa mahiwa wakati yupo shule ya msingi aliwaunganisha watoto wenzie na kuunda kundi la burudani lililotumia vifaa vya kutengeneza wao wenyewe kama malimba, tumba na vimbalama ambavyo walivicheza kama sehemu ya kujifurahisha!

1990 kaka yake mmoja alimnunulia kitolino cha kupuliza(kinanda) hapo alizidi kuupenda muziki.

1995 yeye na wenzie, Mike T, Crazy Doggy, Zay B, Emergency Poison, n.k. ndio wasanii wa kwanza wa muziki wa bongo fleva kufanya onyesho la wazi jukwaani katika mkoa wa iringa ambapo onyesho hilo liliandaliwa na st luis musik center .lilifanyika katika ukumbi wa makosa ulikuwa ukijulikana kama cats hotels kwa sasa ni ukumbi wa IDYDC.