Morogoro Vijijini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Morogoro Vijijini (kijani cheusi) katika mkoa wa Morogoro (kijani) na Tanzania kwa jumla kabla ya kumegwa ili kuanzisha wilaya ya Mvomero.

Wilaya ya Morogoro ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania yenye Postikodi namba 67200.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 263,920 [1]. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 387,736 [2].

Makabila ya wilaya hii ni Waluguru, Wabati, Wakutu, Wandengereko na mengine kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, kama vile Waha, Wasukuma na Wanyaturu.

Morogoro vijijini kuna vijiji vingi vikiwemo Matombo, Mvuha na Kisaki ambavyo vina maliasili nyingi, ikiwemo misitu na madini.

Ni wilaya yenye utajiri mkubwa wa hali ya hewa inayoruhusu mazao yote kustawi: kwa mfano, yale ya joto hustawi maeneo ya bondeni, na ya baridi sehemu za milimani.

Ni chanzo cha mito inayonywesha mikoa ya Dar-es-Salaam na Pwani. Lakini asilimia kubwa ya wakulima hulima bila faida: hubeba mizigo kwenda sokoni kwa umbali mrefu zaidi ya kilometa 25.

Miradi ya umeme inaendelea kushughulikia Morogoro vijijini tofauti na miaka ya nyuma ambapo umeme ulikuwa eneo la Ngerengere jeshini pekee.

Mbali na miradi ya umeme kupitia mpango wa REA, barabara zimeanza kuwekewa lami kwenye maeneo korofi, hivyo kufanya makao makuu ya wilaya kuweza kufikika kwa urahisi kipindi chote cha mwaka.

Shule zina upungufu mkubwa wa walimu, baadhi ya shule huwa vigumu kuzifikia kutokana na miinuko mikali, hivyo kufanya ukaguzi kutokuwepo kabisa au kufanyika mara chache na kupelekea changamoto nyingi kwenye sekta ya elimu ikiwemo walimu kutopenda kufanya kazi kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya Tanzania ya 2002. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2010-10-30.
  2. https://www.nbs.go.tz
Kata za Wilaya ya Morogoro Vijijini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania

Bungu | Bwakira Chini | Bwakira Juu | Gwata | Kasanga | Kibogwa | Kibuko | Kibungo | Kidugalo | Kinole | Kiroka | Kisaki | Kisemu | Kolero | Konde | Lundi | Matuli | Mikese | Mkambalani | Mkulazi | Mkuyuni | Mngazi | Mtombozi | Mvuha | Ngerengere | Selembala | Singisa | Tawa | Tegetero | Tomondo | Tununguo


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morogoro Vijijini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.