Maria Magdalena wa Pazzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maria Magdalena de Pazzi alivyochorwa katika kitabu cha mwaka 1878, Little Pictorial Lives of the Saints.
Njozi ya Mt. Maria Magdalena wa Pazzi ilivyochorwa na Pedro de Moya.

Maria Magdalena wa Pazzi (Firenze, Italia, 2 Aprili 1566 – Firenze 25 Mei 1607) alikuwa mmonaki wa shirika la Wakarmeli ambaye alisali sana kwa ajili ya urekebisho wa Kanisa, alijaliwa karama za pekee na kuongoza wenzake kwenye ukamilifu wa Kikristo[1].

Alipata umaarufu kutokana na ubora wa maisha yake ya sala na toba hata akatangazwa mtakatifu na Papa Klementi IX tarehe 22 Aprili 1669.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka kwenye tarehe ya kifo chake[2].

Sala yake[hariri | hariri chanzo]

Neno, wewe ni wa ajabu katika Roho Mtakatifu pia, ukimfanya ajimimine katika roho hivi kwamba roho inakuja kuungana na Mungu, inamjua Mungu, inamuonja Mungu, haifurahii chochote isipokuwa Mungu.

Na Roho Mtakatifu anakuja rohoni imetiwa daima mhuri azizi ya Damu ya Neno, Mwanakondoo aliyechinjwa; tena damu ndiyo inayomsukuma aje, ingawa mwenyewe anakuja kwa kutaka...

Roho Mtakatifu, huishii katika Baba asiyebadilika, wala huishii katika Neno; ingawa umo daima ndani ya Baba, ndani ya Neno, ndani mwako na ndani ya roho zote zenye heri mbinguni na ndani ya viumbe.

Unahitajiwa na kiumbe kutokana na damu iliyomwagwa na Neno, Mwana pekee, ambaye kwa ari ya upendo amejifanya ahitahiwe na kiumbe chake.

Unapumzika katika viumbe vilivyojiandaa kupokea ndani mwao, kwa kushirikishwa vipaji vyako, mfano wako kwa usafi.

Unapumzika ndani ya wale wanaopokea tunda la damu ya Neno na kujifanya maskani ya kukufaa.

Njoo, Roho Mtakatifu.

Uje muungano na Baba, faraja ya Neno.

Roho wa ukweli, ndiwe tuzo la watakatifu, burudisho la roho, mwanga wa giza, utajiri wa mafukara, hazina ya wenye upendo, shibe ya wenye njaa, faraja ya wanaohiji; basi ndiwe mwenye hazina zote.

Njoo wewe ambaye, kwa kumshukia Maria, ulimfanya Neno awe mwili, fanya tena ndani mwetu kwa neema kile ulichomfanyia Maria kwa neema na maumbile.

Njoo, uliye lishe ya kila wazo safi, chemchemi ya kila wema na fungu la usafi wote.

Njoo, uteketeze ndani mwetu yale yote yanayotufanya tusiweze kuteketea ndani mwako.

Maandishi yake[hariri | hariri chanzo]

  • Mary Magdalen de' Pazzi, The Complete Works of Saint Mary Magdalen de' Pazzi Carmelite and Mystic (1566–1607), 5 vols, translated by Gabriel Pausback, O.Carm., Fatima 1969-1973.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]