Nimonia esinofili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Eosinophilic pneumonia
Mwainisho na taarifa za nje
ICD-10J82.
ICD-9518.3
MedlinePlus000105
MeSHD011657

Nimonia esinofili (EP) ni ugonjwa ambapo aina fulani ya seli nyeupe za damu ziitwazo eosinofili hukusanyika kwenye mapafu. Seli hizi husababisha kuvurugika kwa nafasi za kawaida za hewa (alveoli) ambako oksijeni huzinduliwa kutoka kwa anga. Aina mbalimbali za nimonia esinofili huwepo na zinaweza kutokea katika kundi la umri wowote. Dalili zinazojitokeza sana sana ni pamoja na kikohozi, homa, tatizo la kupumua, na kutokwa na jasho usiku. EP hutambuliwa kwa kutumia mchanganyiko wa dalili mbalimbali, matokeo ya ukaguzi wa afya unaofanywa na mtoa huduma za afya, na matokeo ya vipimo vya damu na eksirei. Ubashiri huwa bora wakati sehemu kubwa ya EP imetambuliwa na matibabu kwa kutumia kotikosteroidi yameanzishwa.

Aina za nimonia esinofili[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa nimonia esinofili umegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na kama kisababishi kinaweza kutambuliwa au la. Visababishi vinavyojulikana ni pamoja na baadhi ya dawa au vichochezi vya kimazingira, maambukizi ya vimelea, na saratani. EP pia inaweza kutokea wakati mfumo wa kinga umeshambulia mapafu, ugonjwa uitwao tatizo la Churg-Strauss. Wakati kisababishi hakipatikani, EP hupachikwa jina la "idiopathiki." EP ya idiopathiki inaweza kugawanywa katika "nimonia esinofili kali" (AEP) na "nimonia esinofili sugu" (CEP) kulingana na dalili ambazo mtu anapata.[1]

Dalili[hariri | hariri chanzo]

Visababishi vingi vya nimonia esinofili vina dalili zinazofanana. Kikohozi, homa, kuongeza kwa tatizo la kupumua, na kutokwa na jasho usiku ni dalili maarufu na hujitokeza kwa karibu kila mtu anayeugua. Nimonia esinofili kali kwa kawaida huendelea kwa kasi sana. Homa na kikohozi zinaweza kutokea wiki moja au mbili tu kabla ya matatizo ya kupumua yameendelea na kufikia hatua ya kushindwa kupumua hivyo basi kuhitaji uingizaji hewa kwa kutumia mitambo. Nimonia esinofili sugu kwa kawaida huendelea polepole. Dalili hujilimbikiza katika kipindi cha miezi kadhaa na huwa ni pamoja na homa, kukohoa, tatizo la kushindwa kupumua, kukorota, na kupungua kwa uzito. Watu walio na CEP mara nyingi hupatikana kuwa na pumu kabla ya CEP hatimaye kutambuliwa.

EP inayotokana na dawa au vitu mbalimbali kwenye mazingira ni sawa na hutokea baada ya kufichuliwa kwa kitu kinachojulikana kusababisha. EP inayotokana na maambukizi ya vimelea ina dalili za mwanzo pamoja na dalili nyingi tofauti zinazohusiana na aina mbalimbali za vimelea vya msingi. EP katika mazingira ya saratani mara nyingi huendeleza katika muktadha wa utambuzi unaojulikana nwa habari ya uvimbe wa kansa, kansa ya kizazi, nk.

Kumekuwa na matukio ya nimonia esinofili kinachosababishwa na madawa kama vile daptomycin (Cubicin). Mbili za kesi hizi zimebainishwa kuwa kesi sugu zinazotegemea steroidi. (Rejea Clinically Infectious 2010:50 (1 Machi) pp735-739.

Pathofisiolojia[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa nimonia esinofili unaweza kuanzia kwa njia nyingi tofauti kulingana na kisababishi chake msingi. Eosinofili zinafikiriwa kuwa na jukumu msingi katika kulinda mwili dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na vimelea. Magonjwa mengi, kama vile pumu na eksema, hutokea wakati eosinofili zinazidi hasa zinapoathiriwa na vichochezi vya kimazingira na kutoa kemikali zilizopita kiasi (sitokini s) kama vile histamini. Sifa ya kawaida miongoni mwa visababishi mbalimbali vya EP ni eosinofili kuzidi au ini kukosa kufanya kazi vizuri.

Madawa na vichochezi vya kimazingira[hariri | hariri chanzo]

Madawa, dawa za Kulevya na vichochezi vya kimazingira vinaweza kuchochea kutofanya kazi vizuri kwa eosinofili. Madawa kama vile NSAIDs (yaani ibuprofen), nitrofurantoin, phenytoin, L-tryptophan, daptomycin[4] na ampicillin na madawa ya kulevya kama vile heroini na kokeini yanayovutwa yanaweza kuchochea mzio unaosababisha EP. Kemikali kama vile salfiti, alumini silikati, na moshi wa sigara zinaweza kusababisha EP wakati zinapovutwa. Mzimamoto kutoka New York alipatwa na EP baada ya kuvuta hewa ya vumbi kutoka Kituo cha Biashara Duniani (World Trade Center) tarehe 11 Septemba 2001.[2]

Maambukizi ya vimelea[hariri | hariri chanzo]

Vimelea husababisha EP kwa njia tatu tofauti. Vimelea vinaweza ama kuvamia mapafu, kuishi katika mapafu kama sehemu ya maisha yao, au kuenea kwa mapafu kupitia damu. Eosinofili huhamia kwenye mapafu ili kupambana na vimelea hivyo na kusababisha EP. Vimelea muhimu vinavyovamia mapafu ni pamoja na Paragonimus minyoo bapa ya mapafu na aina za tegu za Echinococcus na Taenia solium. Vimelea muhimu vinavyoishi kwenye mapafu kama sehemu ya kawaida ya maisha yao ni pamoja na minyoo ya (helminth s) Ascaris lumbricoides, stercoralis Strongyloides na aina za tegu za Ancylostoma duodenale na americanus Necator. Wakati EP imesababishwa na kundi hili la mwisho, mara nyingi huitwa " tatizo la Löffler". Kundi la mwisho la vimelea husababisha EP wakati idadi kubwa ya mayai yamebebwa na damu hadi kwenye mapafu. Vimelea vilivyo katika kundi hili ni pamoja na spiralis Trichinella, stercoralis Strongyloides, Ascaris lumbricoides, tegu, na skistosomu.[3]

AEP na CEP[hariri | hariri chanzo]

Kufikia mwaka wa 2005, visababishi vya aina hizi mbili; AEP na CEP, vilikuwa havijulikani. Kuna tuhuma kuwa angalau AEP husababishwa na majibu ya mwili kwa baadhi ya vichochezi ambavyo havijatambuliwa vya kimazingira.

Uaguzi[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa nimonia esinofili hutambuliwa katika mojawapo ya hali tatu: wakati hesabu kamili ya damu inaonyesha kuongezeka kwa eosinofili na eksirei ya kifua au picha zilizopigwa kwa kompyuta zinabainisha hali isiyo ya kawaida katika mapafu, wakati biopsi inatambua kuongezeka kwa eosinofili katika tishu za mapafu, au wakati eosinofili nyingi zinapatikana katika maji yanayotolewa kwa bronkoskopi (maji ya bronchoalveolar lavage (Bal)). Uhusiano na dawa au saratani kwa kawaida hudhihirika baada ya ukaguzi wa historia ya mtu huyo ya matibabu. Maambukizi maalum ya vimelea hutambuliwa baada ya kuchunguza mfichuo wa mtu kwa vimelea vya kawaida na kufanya vipimo vya kimaabara ili kuangalia vitu vinavyoweza kuwa vimesababisha. Kama hakuna sababu msingi iliyopatikana, utambuzi ya AEP au CEP hufanywa kulingana na vigezo vifuatavyo. Kuna uwezekano mkubwa wa AEP kuambatana na kushindwa kupumua baada ya ugonjwa mkali wa febrili ambao kwa kawaida ni wa chini ya wiki moja, mabadiliko katika maeneo kadhaa na maji katika eneo linalozunguka mapafu kwenye eksirei ya kifua, na eosinofili zilizozidi asilimia 25 kwenye Bal. Hali zingine za kimaabara zisizo za kawaida ni pamoja na ongezeko la idadi ya chembechembe nyeupe za damu, kiwango cha kubakisha mashapo ya erithrositi, na kiwango cha imunoglobulini E. Vipimo vya hali ya ufanyaji kazi wa mapafu kwa kawaida huonyesha mchakato uliozuiwa na ulio na uwezo uliopunguka wa kutawanyika kwa kaboni monoksidi. Uwezekano wa kuwa aina iliyopo ni ya CEP huwa sana sana wakati dalili zimekuwepo kwa zaidi ya mwezi mmoja. Vipimo vya kawaida vya kimaabara vya CEP ni pamoja na kuongezeka kwa eosinofili kwenye damu, kiwango cha juu cha kubakisha mashapo ya erithrositi, anemia inayotokana na upungufu wa chuma, na kuongezeka kwa pletileti. Eksirei ya kifua inaweza kuonyesha hali iliyopo isiyo ya kawaida mahali popote, lakini matokeo maalum zaidi huwa ni kuongezeka kwa kivuli katika periferi ya mapafu, mbali na moyo.

Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Wakati ugonjwa wa nimonia esinofili unahusiana na ugonjwa kama vile saratani au maambukizi ya vimelea, matibabu ya sababu msingi hufanya kazi katika kutatua ugonjwa huu wa mapafu. Hata hivyo, wakati imetokana na AEP au CEP, matibabu kwa kutumia kotikosteroidi husababisha utatuzi wa haraka na wa ghafla wa dalili kwa muda wa siku moja au mbili. Kwa kawaida, ama methylprednisolone ya kudungwa kwenye mishipa au prednisoni ya kumezwa hutumiwa. Katika AEP, kwa kawaida matibabu huendelezwa kwa muda wa mwezi mmoja baada ya dalili kutoweka na eksirei kurejea kawaida (kwa kawaida jumla ya wiki nne). Katika CEP, kwa kawaida matibabu huendelezwa kwa muda wa miezi mitatu baada ya dalili kutoweka na eksirei kurejea kawaida (kwa kawaida jumla ya miezi minne). Steroidi zilizonuswa kama vile fluticasone zimetumika ipasavyo wakati kuacha matumizi ya prednisone za kumezwa kumesababisha kurudi tena kwa ugonjwa.[4] Kwa sababu EP huathiri mapafu, watu walio na EP kuwa na tatizo la kupumua. Kama sehemu kubwa ya mapafu imehusika, haiwezekani kwa mtu kupumua vya kutosha kuishi, bila msaada. Mashine zisizohitaji kuingizwa ndani ya mwili kama vile mashine ya 'bilevel positive airway pressure' zinaweza kutumika. Vinginevyo, kuwekwa wa bomba la kupumua katika mdomo kunaweza kuwa jambo la lazima na kipitisha hewa kinaweza kutumika kumsaidia mtu huyo kupumua.

Ubashiri[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa wa nimonia esinofili unaotokana na saratani au maambukizi ya vimelea hubeba ubashiri unaohusiana na ugonjwa msingi. Hata hivyo, AEP na CEP, huwa na uwezo mdogo sana unaohusiana wa kufa bora tu uangalifu kwa makini unapatikana na matibabu kwa kutumia kotikosteroidi unatolewa. Mara nyingi CEP hurudi tena wakati matumizi ya prednisone yameachwa, kwa hiyo, baadhi ya watu wenye CEP huhitaji tiba ya maisha. Prednisoni sugu huhusishwa na madhara mengi, ikiwa ni pamoja na maambukizi kuongezeka, mifupa dhaifu, vidonda vya tumbo, na mabadiliko ya sura.[5]

Epidemiolojia[hariri | hariri chanzo]

Nimonia esinofili ni ugonjwa unaojitokeza kwa nadra. Visababishi vya vimelea hudhihirika sana katika maeneo ya kijiografia ambapo kila kimelea kimeenea. AEP inaweza kutokea katika umri wowote, hata katika watoto ambao hapo awali walikuwa na afya, ingawa wagonjwa wengi huwa na umri kati ya miaka 20 na 40. Takriban wanaume wawili kwa kila mwanamke mmoja huathiriwa. AEP imehusishwa na uvutaji sigara. CEP hutokea sana katika wanawake ikilinganishwa na wanaume na haionekani kuhusiana kwa vyovyoye na uvutaji sigara. Kumekuwa na uhusiano fulani na mionzi ya saratani ya matiti umeelezewa.[6]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Aina sugu ya nimonia esinofili ilieezewa kwa mara ya kwanza na Carrington[7] katika mwaka wa 1969, na pia inajulikana kama tatizo la Carrington. Kabla ya wakati huo, nimonia esinofili ulikuwa ugonjwa ulioelezewa vizuri na kwa kawaida ulihusishwa na madawa au vichochezi vya vimelea. Aina kali ya nimonia esinofili ilielezewa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1989[8][9]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Bain GA, Flower CD (1996). "Pulmonary eosinophilia". Eur J Radiol 23 (1): 3–8. doi:10.1016/0720-048X(96)01029-7 . PMID 8872069 . http://linkinghub.elsevier.com/retrieve/pii/0720048X96010297.
 2. Rom WN, Weiden M, Garcia R, et al. (2002). "Acute eosinophilic pneumonia in a New York City firefighter exposed to World Trade Center dust". Am. J. Respir. Crit. Care Med. 166 (6): 797–800. doi:10.1164/rccm.200206-576OC . PMID 12231487 . http://ajrccm.atsjournals.org/cgi/pmidlookup?view=long&pmid=12231487.
 3. Weller PF (1994). "Parasitic pneumonias", in Pennington, James: Respiratory infections: diagnosis and management, 3rd, New York: Raven Press, 695. ISBN 0-7817-0173-2. 
 4. Jantz MA, Sahn SA (1999). "Corticosteroids in acute respiratory failure". Am. J. Respir. Crit. Care Med. 160 (4): 1079–100. PMID 10508792 . http://ajrccm.atsjournals.org/cgi/pmidlookup?view=long&pmid=10508792.
 5. Naughton M, Fahy J, FitzGerald MX (1993). "Chronic eosinophilic pneumonia. A long-term follow-up of 12 patients". Chest 103 (1): 162–5. doi:10.1378/chest.103.1.162 . PMID 8031327 .
 6. Cottin V, Frognier R, Monnot H, Levy A, DeVuyst P, Cordier JF (2004). "Chronic eosinophilic pneumonia after radiation therapy for breast cancer". Eur. Respir. J. 23 (1): 9–13. doi:10.1183/09031936.03.00071303 . PMID 14738224 . http://erj.ersjournals.com/cgi/pmidlookup?view=long&pmid=14738224.
 7. Carrington CB, Addington WW, Goff AM, et al. (1969). "Chronic eosinophilic pneumonia". N. Engl. J. Med. 280 (15): 787–98. doi:10.1056/NEJM196904102801501 . PMID 5773637 .
 8. Badesch DB, King TE, Schwarz MI (1989). "Acute eosinophilic pneumonia: a hypersensitivity phenomenon?". Am. Rev. Respir. Dis. 139 (1): 249–52. PMID 2912347 .
 9. Allen JN, Pacht ER, Gadek JE, Davis WB (1989). "Acute eosinophilic pneumonia as a reversible cause of noninfectious respiratory failure". N. Engl. J. Med. 321 (9): 569–74. doi:10.1056/NEJM198908313210903 . PMID 2761601 .

Pia Tazama[hariri | hariri chanzo]

 • Nimonia
 • Pumu
 • Nimonia inayosababishwa na vimelea