Nottingham Evening Post

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Nottingham Evening Post
Jumba la Castle Wharf, makao makuu ya Nottingham Evening Post tangu Machi 1998
Jina la gazeti Nottingham Evening Post
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila siku
*. Gazeti la Jumatatu mpaka Jumamosi
*. Toleo la asubuhi
Toleo la "mwisho"
Eneo la kuchapishwa Nottingham
Nottinghamshire
Derbyshire: kama vile Long Eaton na Sandiacre.
Nchi Uingereza
Mwanzilishi Thomas Forman
Mhariri *. Graham Glen - alistaafu Agosti 2006
*. Malcolm Phelby
Mmiliki Kundi la Newspapers Northcliffe Group
Makao Makuu ya kampuni Castle Wharf
Nakala zinazosambazwa takriban 55,500 kila siku.
Machapisho husika *. The Football Post
*. Bygones
Tovuti 'http://www.thisisnottingham.co.uk/

/pre> Nottingham Evening Post ni gazeti la Uingereza ambalo huchapishwa katika eneo la Nottingham, Nottinghamshire na maeneo tofauti ya Derbyshire kama vile Long Eaton na Sandiacre. Posthuchapishwa kila wiki kutoka Jumatatu mpaka Jumamosi huku matoleo mawili yakichapishwa kila siku: toleo la asubuhi na toleo la "mwisho". Bei yake ni 35p, lakini kwa jumla ni 39p kama mtu anataka gazeti lifikishwe hadi mlangoni mwake. Jarida hili linamilikiwa na kundi la Newspapers Northcliffe Group, ambalo ni sehemu ya Daily Mail & General Trust, na lilikuwa "Gazeti la kupigia kampeni la mwaka".

Mara nyingine gazeti hili huhusisha makala spesheli ambayo yanayojumuisha malengo ama sehemu mbalimbali za maisha katika eneo la Nottingham. Mfano wa makala kama haya ni makala ya mfululizo kuhusu Waislamu katika Nottingham (Muslims in Nottingham) katika mwezi wa Aprili 2007. Makala haya yalihusisha mahojiano na makala mfululizo kwa wiki moja katika gazeti na pia katika tovuti yao ya Evening Post. Wao waliilenga jamii ya Waislamu katika eneo la Nottingham wakiwapa fursa ya kutoa maoni yao kuhusu maisha mjini humo.

Toleo la kwanza la Evening Post lilichapishwa na Thomas Forman mnamo 1 Mei 1878. Liliuzwa kwa bei ya ½ d na lilikuwa na urefu wa kurasa nne.

Mnamo Machi 1996, Post lilianzishwa upya tena kama gazeti la rangi zote lililochapishwa katika mtindo wa gazeti dogo. Ingawaje, gazeti la Jumamosi lilikuwa limechapishwa katika mtindo uo huo tangu mwaka wa 1982.

Gazeti la Post lilikuwa na ofisi zake katika barabara ya Forman Street ,iliyo katikati mwa Nottingham, hadi mwaka wa 1998. Katika mwaka wa 1998, lilihamia Castle Wharf.

Licha ya kuchapisha gazeti kuu, Post huchapisha gazeti la michezo,The Football Post, kila Jumamosi katika msimu wa soka. Hili huhusisha machapisho kuhusu vilabu viwili vya mji wa Nottingham vilivyo katika ligi ya Football League(Nottingham Forest na Notts County). Vilevile kuna makala ya kandanda ya mitaani isiyo ya ligi, kriketi, mchezo wa magongo kwenye barafu na mchezo wa raga. Zaidi ya hayo, Post lilichapisha hapo awali jarida la Forest Fever ambalo lililokuwa la kila wiki likichapisha masuala mbalimbali ya klabu ya Nottingham Forest Football Club. Makala yake ya kindani kuhusu matukio katika The City Ground yalihusu mahojiano na wanakandanda wa sasa, wanakandanda wa awali, usimamizi na wafuasi wa kilabu chao.

Pia, kuna jarida la kila mwezi,Bygones, linalochapisha makala na hadithi haswa juu ya historia ya Nottingham.

Mhariri wa awali wa Evening Post ,Graham Glen, alistaafu mnamo Agosti 2006. Mhariri wa sasa ni Malcolm Phelby na usambazaji wa magazeti haya ni takriban 55,500 kila siku.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]