UNESCO-IHE

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

UNESCO-IHE ni kifupi cha "United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization - Institute for Hydrological Education", au Taasisi ya Elimu ya Maji ya UNESCO.

Ni taasisi ya kimataifa kwa ajili ya elimu ya maji iliyoanzishwa rasmi mwaka 2003. UNESCO-IHE inaendeleza kazi iliyoanzishwa na IHE mwaka 1957. Wakati huo IHE ilikuwa ikitoa stashahada ya juu katika fani ya uhandisi wa maji na utaalamu wa kiufundi kwa nchi zinazoendelea.

Taasisi ya Kimataifa ya maji, UNESCO-IHE ipo katika mji wa Delft nchini Uholanzi (Netherlands), na inamilikiwa na nchi zote wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Ilianzishwa kama taasisi la daraja la kwanza kwa mujibu wa UNESCO kwa ushirikiano na Serikali ya Uholanzi.

Ni taasisi kubwa zaidi ya elimu ya maji duniani, na taasisi pekee katika mfumo wa Umoja wa Mataifa iliyopewa mamlaka ya kutoa shahada za uzamili katika sayansi.

Majukumu ya UNESCO-IHE yanaainishwa kama ifuatavyo :

  • Ina jukumu la uongozi wa Kimataifa katika kuweka viwango na kuandaa mipango ya elimu ya stashada ya juu katika elimu ya maji na kuendeleza mafunzo ya kitaalamu;
  • Kujenga uwezo wa kitalaamu kwa nchi zinazoendelea;
  • Kutoa elimu, mafunzo na mipango ya utafiti.
  • Kuweka misingi na kusimamia mitandao ya kielimu ya taasisi na mashirika katika sekta ya maji duniani kote;
  • Kutumika kama 'jukwa la sera' kwa nchi shirika za Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na washikadau wengine; na
  • Kutoa utaalam na ushauri wa kitaalamu kuhusu elimu ya maji.

Tangu ianzishwe mwaka 1957, taasisi ya IHE -kama ilivyojulikana- imeshatoa stashahada kwa wataalamu(wahandisi na wanasayansi) zaidi ya elfu kumi na nne( 14,000) wengi wao kutoka nchi zinazoendelea, za mpito zinazowakilisha nchi mia moja na sitini(160) (Wahandisi na wanasayansi) karibu kabisa kutoka zinazoendelea / mpito ya nchi, anayewakilisha 160 nchi. Na imeshatunuku shahada ya falsafa (PhD) kwa watahini za sabini na tano(75),na kufanya utafiti mblimbali na kujenga uwezo wa kitaalamu katika miradi duniani kote.