Henry Rono

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Henry Rono
Rekodi za medali
Wanaume Wakimbiaji
Anawakilisha nchi Bendera ya Kenya Kenya
Michezo ya All-Africa
Dhahabu 1978 Algiers 10,000 m
Dhahabu 1978 Algiers 3,000 m steeplechase

Henry Rono (Kapsabet, 12 Februari 1952 - 15 Februari 2024) ni mkimbiaji wa zamani kutoka nchi ya Kenya.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Rono alizaliwa katika sehemu ya Milima ya Nandi nchini Kenya na kabila yake ni Kinandi. Alianza mbio akiwa angali katika shule ya msingi. Kuanzia mwaka wa 1977 alihudhuria Chuo Kikuu cha Washington State, pamoja mkimbiaji mwenzake Samson Kimobwa, ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mita 10,000 mwaka wa 1977. Mkufunzi wake katika chuo kikuu alikuwa John Chaplin. Wakimbiaji zaidi kutoka nchi ya Kenya baadaye walijiandikisha katika chuo kikuu cha Washington State, pamoja na Bernard Lagat, Mike Kosgei, na Patrick Muturi. Akiwa angali bado katika chuo kikuu cha Washington State, Rono akawa mtu wa tatu tu katika historia (baada ya Gerry Lindgren na Steve Prefontaine) kushinda mchuano wa Cross Country wa wanaume wa NCAA mara tatu, katika miaka ya 1976, 1977, na 1979. Muda wake wa ushindi ulikuwa 28:07 mwaka wa 1976 na muda wake umebakia wa kasi zaidi katika mita 10,000 ya cross-country katika historia ya NCAA (ingawa mwaka wa 2008 Galen Rupp alikimbia kwa muda wa 27:41 katika mkutano wa mkoa wa NCAA katika kozi ambayo ilisemekana kuwa mita 80 fupi kuliko mpimo wa kawaida ). Pia alikuwa bingwa mtetezi wa steeplechase ya NCAA miaka ya 1978 na 1979 na bingwa wa mchuano wa ndani (yaani indoor kwa lugha ya kimombo) wa NCAA katika mita 3000 mnamo mwaka wa 1977.

Upeo wa wasifu wa kukimbia wa Rono ulikuwa katika msimu wa mwaka 1978. Katika muda wa siku 81 tu, alivunja rekodi nne za dunia: ya mita 10,000 (27:22.5), ya mita 5,000 (13:08.4), steeplechase ya mita 3,000 (8:05.4), na mita 3,000 (7:32.1 ); mafanikio ambayo hayajafikiwa kamwe katika historia ya mbio za masafa marefu. Alipunguza rekodi ya mita 10,000 kwa karibu sekunde 8, ya mita 5000 na 4.5, ya steeplechase na 2.6, na 3000 kwa sekunde tatu kamili. Katika mwaka huo huo pia alishinda medali za dhahabu katika mbio za mita 5000 na 3000 m huku akaishiriki katika Michezo ya Jumuiya ya Madola. Kati yake tendaji zake zingine zilikuwa steeplechase ya mita 5000 mara mbili katika siku moja katika michuano ya kufuzu ya NCAA katika Chuo Kikuu cha Oregon katika uwanja wa Eugene 's Hayward. Aliweka rekodi katika matukio yote mawili, na muda wake katika matukio yote mawili yaalikuwa 8:18 na 13:22 mtawalia. Muda wa 8.18 ulipunguza rekodi ya NCAA kwa sekunde 6. Wakati alishiriki katika fainali ya mbio ya steeplechase siku iliyofuata, alishinda kwa muda wa 8:12.39, na kupunguza rekodi ya mkutano wa NCAA tena kwa muda wa sekunde sita. Alishinda medali za dhahabu katika mbio za mita 10,000 na mita 3000 katika Michezo ya All-Africa mwaka wa 1978.

Ingawa hakutamalaki sana kama alivyotamalaki mwaka wa 1978, Rono aliendelea kukimbia na kushindana katika viwango vya juu kwa miaka minne ijayo, na kukimbia kwa muda wa kasi zaidi (13:19) wa mwaka katika mbio za mita 5,000 na kushinda mchuano wa cross-country wa NCAA mwaka wa 1979; hii ilikuwa mojawapo ya mbio za kasi zaidi katika historia ya mbio za mita 10,000 mwaka huo 1980 (27:31), huku alikuwa amekuwa na mwaka wa nguvu katika mbio ya mita 5000 na alikuwa na rekodi nyingine ya dunia mwaka wa 1981, na kukimbia muda wa kasi zaidi wa tatu katika historia katika mbio ya mita 5,000 (13:08.9) na vilevile mara mbili alimaliza mbio yak echini ya muda wa 27:30 na kukaribia rekodi ya dunia mita 10,000 kwa sekundi chache mwaka wa 1982. Baada ya 1978 mafanikio yake yakawa si ya mara kwa mara, kwani aliathiriwa na matatizo ya kuongeza uzito na kunywa pombe ambayo hakumwezeaha kukimbia kwa kasi. Mwaka wa 1981, alikimbia mbio za hali ya juu katika mita 5,000 na alivunja rekodi yake ya dunia ya mita 5,000 msimu wa majira ya joto ukielekea kuisha kwa muda wa 13:06.20, baada ya kuripotiwa kuwa alitumia sehemu bora ya siku akipumzika ilikupunguza ulevi alikuwa ameupata usiku kabla. Rono hakupata fursa ya kushiriki katika Michezo ya Olimpiki, kwani nchi yake iligoma kushiriki katika Michezo ya Olimpiki ya miaka ya 1976 na 1980 na kufikia mwaka wa 1984 alikuwa ameacha kushiriki.

Baada ya kustaafu kwake, mbali na kukabiliwa na ulevi, hakuwa na mpango wa kutumia mapato yake (kamwe hakuwa na wakala au mshauri wa kifedha). Baadaye akawa maskini hohehahe, katika miaka ya 1990, alitumia muda mwingi katika makazi ya wasiokuwa na makazi katika mji mkuu wa Washington DC.

Rekodi yake ya dunia (8:05.4) ya steeplechase ya mita 3,000 m wake ilisimama kwa miaka 11, na, kuanzia mwaka wa 2008, bado inasimama kama rekodi ya NCAA.

Leo, Rono ni mlevi anayejirekebisha na ni mkufunzi katika shule ya sekondari katika kukimbia katika sehemu ya Albuquerque, New Mexico na anasoma ilikuhitimu na shahada katika elimu maalum. Alipohitimu umri wa miaka 55 mwezi Februari mwaka wa 2007, Rono alijaribu kuvunja rekodi ya dunia ya world masters mile ya wakimbiaji wenye umri wa 55 hadi 59. Pia aliandika tawasifu yake, inayoitwa Olimpic Dream , mwaka wa 2007.

Mwaka wa 2009 iliripotiwa kuwa alipoteza uwasiliano na mke wake Jennifer Jepkemboi na watoto wake wawili Maureen Kipkorir na Calvin Chepchumba, na anajaribu kuwasiliana nao.

Ubora wa binafsi[hariri | hariri chanzo]

  • Mita 3000 - 7:32.1 (1978)
  • Mita 5000 - 13:06.20 (1981)
  • Mita 10,000 - 27:22.47 (1978)
  • Mita 3000 Steeplechase 8:05.4 (1978)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Records
Alitanguliwa na
United Kingdom Brendan Foster
Men's 3,000 m World Record Holder
27 Juni 1978 – 20 Agosti 1989
Akafuatiwa na
Moroko Said Aouita
Alitanguliwa na
New Zealand Dick Quax
Men's 5000m World Record Holder
8 Aprili 1978 – 7 Julai 1982
Akafuatiwa na
United Kingdom David Moorcroft
Alitanguliwa na
Kenya Samson Kimobwa
Men's 10,000 m World Record Holder
11 Juni 1978 – 2 Julai 1984
Akafuatiwa na
Ureno Fernando Mamede
Alitanguliwa na
Uswidi Anders Gärderud
Men's Steeplechase World Record Holder
13 Mei 1978 – 3 Julai 1989
Akafuatiwa na
Kenya Peter Koech
Awards
Alitanguliwa na
Kuba Alberto Juantorena
United Press International
Athlete of the Year

1978
Akafuatiwa na
United Kingdom Sebastian Coe
Alitanguliwa na
Kuba Alberto Juantorena
Men's Track & Field Athlete of the Year
1978
Akafuatiwa na
United Kingdom Sebastian Coe
Sporting positions
Alitanguliwa na
West Germany Karl Fleschen
Men's 3,000 m Best Year Performance
1978
Akafuatiwa na
Marekani Rudy Chapa
Alitanguliwa na
New Zealand Dick Quax
Men's 5,000 m Best Year Performance
1978
Akafuatiwa na
Tanzania Suleiman Nyambui
Alitanguliwa na
Ethiopia Miruts Yifter
Men's 5,000 m Best Year Performance
1981
Akafuatiwa na
United Kingdom David Moorcroft
Alitanguliwa na
West Germany Michael Karst
Men's 3,000 m Steeple Best Year Performance
1978 — 1979
Akafuatiwa na
Poland Bronisław Malinowski