Royal York

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Royal York
Habari ya Jumla
Jiji: Toronto, Ontario Kanada, M5J 1E3
Hali yake: Ujenzi Umemalizika
Mwaka wa Ujenzi: 1929
Magorofa: 19
Wataalam husika:
Ross & Macdonald; Sproatt & Rolph
Fairmont Royal York inavyonekana kutoka juu ya Jengo la CN Tower.

Hoteli ya Fairmont Royal York (hujulikana kwa kawaida kama "Royal York"), ilijulikana hapo zamani kama Hoteli ya Royal York, ni hoteli kubwa na yenye historia katika eneo la Toronto,Ontario nchini Kanada katika barabara ya 100 Front Street West.

Ilifunguliwa tarehe 11 Juni 1929, mipango ya Royal York ilichorwa na kupangwa na wataalamu wa kazi hiyo Ross na Macdonald(pamoja na Sproatt na Rolph) na ikajengwa na shirika la reli la Canadian Pacific Railway karibu na stesheni ya Union Station. Likiwa ma magorofa 28, jengo hilo lenye muundo wa Château lilikuwa jengo kubwa kabisa katika ufalme wa Uingereza mpaka walipojenga mnara wa Benki ya Kanada jijini Toronto kwenye barabara ya King Street.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hoteli hii ilikuwa hoteli ya tatu kujengwa katika kipande hicho cha ardhi. Katika mwaka wa 1843, hoteli ya Ontario Terrace ilifunguliwa katika kipande hiki cha ardhi na ikaitwa Hoteli ya Sword hapo baadaye, katika mwaka wa 1853. Hoteli hiyo ilibadilishwa jina tena ikawa Revere House na kisha Hoteli ya Queen katika mwaka wa 1862. Kabla ya kubomolewa kwa hoteli hiyo, Hoteli ya Queen ilikuwa mojawapo ya hoteli bora sana jijini Toronto. Hoteli hiyo ilimilikiwa na Winnett na McGaw. Winnett na McGaw walikuwa wamiliki wa hoteli nyingi katika upande wa juu wa Kanada hapo mwanzoni mwa karne ya ishirini. Walimiliki Hoteli ya Queens Royal (Niagara) na walikuwa washirika katika usimamizi wa Tecumsie House huko London , Ontario. Henry Winnett alinunua hisa zote za Dick McGaw za hoteli baada ya kifo chake. Hatimaye , Hoteli ya Queen iliuziwa shirika la reli la Canadian Pacific Railway kisha shirika hilo likabomoa hoteli hiyo ili kujenga Royal York. Thomas Dick McGaw na Henry Winnett walizikwa katika pahali pa kuzikwa pa Mt. Pleasant pamoja na watu kadhaa wa jamaa yao.

Ilipojengwa, ilikuwa hoteli iliyokuwa imeendelea kiteknolojia huku ikiwa na eleveta kumi, redio katika vyumba vyote 1048 na bafu ya kibinafsi katika kila chumba. Ilihusisha ,pia, ukumbi mkubwa uliokuwa na ala kubwa ya muziki ya aina ya pipe organ, Casavant Frères. Ala hiyo ilikuwa kubwa kabisa ya aina yake nchini Kanada. Bodi ya upokeaji simu ilikuwa futi 66 kwa urefu na ulihitaji waendeshaji 35 kuiendesha. Hoteli ilipanuliwa katika mwaka wa 1959 kwa kuongezwa kwa upande wa mashariki ikawa na vyumba 1600 na ikawa hoteli kubwa kabisa katika maeneo ya Jumuiya ya Madola kwa miaka mingi.

Hoteli imekuwa makazi kwa Malkia Elizabeth II na wanachama wengine wa familia ya kifalme ya Kanada wanapozuru Toronto. Malkia hutumia gorofa moja zima akiwa yeye na wafanyikazi wake, yeye hulala katika chumba cha Royal Suite.

Baada ya Hoteli za Fairmont kununua Hoteli za Kanada Pacific, iliamua kutumia jina lake la "Fairmont" katika hoteli zake zote. Kukawa na kilio cha umma dhidi ya kutoa kwa bango la kihistoria la "Royal York" na kuweka lile jipya la "Fairmont". Kama matokeo ya kilio hicho, bango la "Fairmont Royal York" likawekwa likihusisha majina yote mawili.

Mfumo wa barabara iliyo chini ya ardhi wa PATH hutumika kuunganisha hoteli hiyo na Royal Bank Plaza na stesheni ya Union Station.

Chai ya rangi ya kijani kibichi ya Ujapani huwa chakula spesheli katika hoteli hii na hupatikana katika kila chumba.

Nyuki[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Julai 2008, Royal York iliweka mizinga mitatu katika gorofa lake la 13 ili nyuki watumikie shamba dogo lililokuwa katika gorofa hilo. Shamba hilo hutumikia mikahawa tisa kwa kuiuzia mboga na maua. Malkia watatu nyuki na nyuki 40000 wa kazi huzalisha paundi 700 za asali. Hoteli waliipa majina mizinga hiyo mitatu haswa,- Honey Moon Suite, Royal Sweet na V.I. Bee Suite.

Angalia Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ canada.com, Toronto hotel producing its own honey
  2. ^ reuters.com, Toronto hotel boasts own honey from rooftop hives
Alitanguliwa na
Sterling Tower
Jengo Refu Kabisa Jijini Toronto
1929-1931
124m
Akafuatiwa na
Commerce Court North
Alitanguliwa na
Old Royal Bank Building, Montreal
Jengo Refu Kabisa Jijini Toronto
1929—1931
124m
Akafuatiwa na
Commerce Court North