Vifaa vya Deni (Soko la Hisa la Nairobi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kifaa cha deni ni mkopo. Mwombaji hutoa ahadi ya kulipa riba fulani kila robo au nusu mwaka kuanzia tarehe fulani baada ya kupata mkopo huo na pia uahidi kulipa mkopo uliopewa. Hivyo basi, faida kutoka kwa kifaa cha deni hutokana na riba. Kwa sasa hivi, vifaa kadhaa za deni vina kiwango cha riba cha asilimia 14, 12, 01, 8 kutegemeana na aina ya kifaa hicho na siku kiliyosajiliwa. Katika Soko la Hisa la Nairobi waweza kununua na kuuza vifaa vya deni.

Elezo la kifaa cha deni ya kampuni ya Kengen

Ni nani anayeweza kuomba fedha[hariri | hariri chanzo]

Nchini Kenya, makampuni na serikali ndiyo yanaweza kuomba fedha kupitia vifaa vya deni katika soko la hisa. Katika masoko mengine ya hisa, hospitali, vyuo vikuu, mashule na vyama vinaweza kuomba fedha kupitia njia hii ikiwa wanaaminiwa na umma.

Kununua kifaa cha deni[hariri | hariri chanzo]

Katika Soko la Hisa la Nairobi bei ya chini zaidi ya kununua kifaa cha deni ni KShs. 100,000. Unaponunua kifaa cha deni cha kampuni fulani, basi wewe huwa umekopesha kampuni hiyo fedha iliyosambamba na bei ya vifaa vya deni ulivyonunua.

Ni nani anayeweza kununua[hariri | hariri chanzo]

Mtu yeyote wa kibinafsi, Kampuni ya Uwekezaji, Kanisa, Shule, Chuo Kikuu, Kampuni ya Bima na idara nyingine nyingi.

Kuuza kifaa cha deni[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa mahitaji ya kighafla, mwekezaji anaweza kuuza vifaa vya deni alivyonunua katika soko kwa urahisi kwani faida ya kifaa cha deni huongezeka kila siku hivyo basi huwa na bei mpya kila siku. Hivyo basi, mwekezaji anaweza kuuza vifaa vyake vya deni siku yoyote kabla ya siku yake ya kukomaa bila kutozwa faini yoyote.

Hata hivyo, panapokuwa na wauzaji wengi katika soko, bei ya vifaa vya deni hushuka na kisha kupanda wanapopungua.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Faili:Infra bond.jpg
Waziri mkuu wa Kenya akutana na mabroka kutoa kifaa cha deni cha serikali cha ujenzi wa barabara

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]