Edi Gathegi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Edi Gathegi

Edi Mue Gathegi (alizaliwa 10 Machi 1979) ni muigizaji wa filamu na jukwaani kutoka Kenya na Marekani. Anatambulika zaidi kama Dr. Jeffrey Cole (aka "Big Love") kwenye maigizo ya televisheni House, vilevile kama Cheese kwenye filamu ya mwaka 2007 Gone Baby Gone na kama Laurent kwenye filamu za Twilight na New Moon.

Maisha ya utotoni[hariri | hariri chanzo]

Ingawa alizaliwa jijini Nairobi, Kenya, Gathegi alikulia Albany, California.[1] Kabla ya kutunukiwa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara ,alijishughulisha sana na kucheza mpira wa kikapu na aliucheza vizuri mpaka pale alipoumia goti lake;Hali hii ilimutamausha kwa hivyo alianza masomo ya uigizaji kama "kozi rahisi". Hapo ndipo aligundua penzi lake katika taaluma ya uigizaji.[1] Baada alijiunga na Tisch School of the Arts akiwa katika Chuo Kikuu cha New York akisomea kozi ya baad ya kufuzu ya uigizaji.[1] Kazi ya Gathegi katika taaluma ya uigizaji ilianzia kwenye maigizo[2] baadhi ya mafanikio yake kwenye uigizaji ni pamoja na Two Trains Running michezo iliyoigizwa huko Old Globe Theatre, As You Like It, Twelfth Night,Othello, A Midsummer Night's Dream, na Cyrano de Bergerac, miongoni mwa maigizo mengine.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Mara ya kwanza Gathegi kuwa na jukumu la nafasi ya kuigiza kama mtaalamu ni kwenye filamu ya Haitian Cabbie mwaka 2006 Crank .Ingawa awali alikuwa amejaribwa kuigza sehemu ya muhusika Kaylo, maprodiusa walimpatia Efren Ramirez nafasi hiyo na badala yake wakampa Gathegi nafasi ya kuigiza kam Haitian Cabbie.[2] Mwanzo alipinga wazo la yey kuigiza lafudhi ya Haiti lakini alifunzwa na rafiki yake kutoka Haitian.[2] Mwaka 2007 baada ya kuigiza kama muhusika mkuu katika Lincoln Heights na Veronica Mars, Gathegi alikuwa muigizaji maarufu alipoigiza kama Bodie katika Death Sentence , Darudi in The Fifth Patient na kama Cheese katika Gone Baby Gone .Baadaye aliigiza mara kwa mara kama Mormon Intern Dr Jeffrey Cole kwenye igizo la televisheni lililohusu magonjwa na tiba House , na muigizaji mgeni [10] [11] na Life on Mars mwaka 2008 kabla ya kuigiza kama Laurent katika Twilight . kwa mara ya kwanza Gatheji alipojaribiwa kwenye filamu ya mwaka 2008, iliyotokana na jina la kitabu cha kwanza kwenye msururu wa pragramu za televisheni za Stephenie Meyer Twilight Series, alikuwa bado hajasikia kkuhusu mfululizo wa maigizo hayo na wala hakujua kwamaba angeigiza kama mzimu wa kutisha.[3] kwa sasa amesoma mfululizo wote na yeye hujiita kama shabiki sugu.[3][4]

Gathegi aliigiza kama naibu wa Martin kwenye filamu ya My Bloody Valentine 3D ya mwaka 2009.[1] Ananuia kuongoza kwenye toleo la chimbuko pana la filamu kwa jina Joe Turner's Njoo na Gone na pia alirejea nafasi yake kama Laurent katika filamu ya Twilight na New Moon.|chimbuko pana la filamu kwa jina Joe Turner's Come and Gone na pia alirejea nafasi yake kama Laurent katika filamu ya Twilight na New Moon.[5]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

mwaka Anwani Dhima Vidokezo
2006 Crank Haitian Cabbie
2007 House Dr Jeffrey Cole TV series
Gone Baby Gone Cheese
The Fifth Patient Darudi
Death Sentence Bodie
Lincoln Heights Boa TV series
2008 Twilight Laurent
2009 My Bloody Valentine 3D Naibu Martin
The Twilight Saga: New Moon Laurent

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Cassandra Handley (4 Novemba 2008). Q&A: Twilight's Edi Gathegi. Vanity Fair. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-11-09. Iliwekwa mnamo 2008-11-06.
  2. 2.0 2.1 2.2 Twilight Lexicon Q&A with Edi Gathegi. TwilightLexicon.com (10 Machi 2008). Iliwekwa mnamo 2008-11-06.
  3. 3.0 3.1 Denise Martin (28 Oktoba 2008). 'Twilight' Countdown: Edi Gathegi's vampire love. Los Angeles Times. Iliwekwa mnamo 2008-11-10.
  4. Sara Castillo (4 Agosti 2008). We Speak with 'Twilight's' Jacob and Laurent!. FearNet.com. Iliwekwa mnamo 2008-11-10.
  5. Adam B. Vary (30 Januari 2009). 'Twilight' stars, Dakota Fanning talk 'New Moon'. Entertainment Weekly. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-02-03. Iliwekwa mnamo 2009-01-31.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]