Elimu nchini Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanafunzi darasani; sehemu ya Mto Athi, Kenya

Elimu nchini Kenya imekuwa ikizingatia mfumo wa 8-4-4 tangu mwishoni mwa miaka ya 1980, ikiwa ni miaka minane ya elimu ya msingi, ikifuatiwa na miaka minne ya shule ya upili, kisha miaka minne ya chuo au chuo kikuu.

Mbali na haya, kuna sekta kubwa ya shule za binafsi ambazo hushughulikia watu wa viwango vya maisha ya kadri na ya juu, ambao kwa ujumla hufuata mfumo wa elimu ya Uingereza wa elimu ya sekondari na msingi.

Kati ya watoto wote nchini Kenya, asilimia 85 huudhuria shule za msingi, asilimia 24 huudhuria shule za upili na asilimia 2 hujiunga na taasisi za elimu ya juu.

Elimu ya Msingi[hariri | hariri chanzo]

Nairobi Primary school ilianzishwa mwaka 1902.

Kuna aina tatu ya shule za msingi: shule za kutwa ambazo zinajumuisha shule nyingi za msingi; shule za bweni ambazo zimegawanywa katika vitango vitatu: vya gharama ya chini, ya wastani na ya juu; na shule za maeneo kame.

Elimu ya msingi katika shule za msingi za serikali ilifanywa kuwa ya bure na ya kila mmoja (bali si ya lazima) mwezi Januari mwaka wa 2003.

Mfumo wa Harambee huchangia pakubwa katika utoaji wa elimu ya shule za msingi nchini Kenya. (Katika Kiswahili, neno Harambee humaanisha "kuungana pamoja".) Mfumo wa Harambee hugharamia takriban asilimia 75 ya shule za msingi nchini Kenya.

Mtihani wa kitaifa wa shule za msingi nchini enya hufanywa mwishoni mwa masomo ya msingi.

Kimani Maruge, ambaye ni Mkenya, ndiye aliyekuwa mtu mkongwe zaidi ulimwenguni kujiunga na shule ya msingi .Ni mkulima ambaye hakuwa amesoma, alijisajili akiwa na miaka 84 baada ya kufahamu kuwa masomo ya msingi yalikuwa ya bure. Alifariki mwaka wa 2009 akiwa na umri wa miaka 89.[1]

Elimu ya Shule za Upili[hariri | hariri chanzo]

Wanafunzi nchini Kenya katika shule za sekondari huchukua miaka minne kujiandaa kwa masomo ya vyuo. Wanafunzi wengi huanza kuyajenga maisha yao ya usoni kwa kujiendeleza katika masomo yatakayowapa kazi. Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne hufanywa mwishoni mwa masomo ya shule ya upili. Mnamo mwaka wa 2008, serikali ilianzisha mpango wa kutoa elimu ya bure kwa shule za upili.

Kuna vitengo vitatu vya shule za sekondari: shule za binafsi, shule zinazofadhiwa na serikali na shule za harambee. Shule zinazofadhiliwa na serikali zina ushindano mkali unaopelekea mmoja kati ya watoto wanne kukubaliwa kujiunga nazo. Kujiunga na shule ya upili hutegemea alama za mwanafunzi katika mtihani wake wa darasa la nane (K.C.P.E). Shule nyingi zinazofadhiliwa na serikali ni za bweni .

Shule za harambee hazina ushindani mkali na zinajumuisha asilimia 75 ya shule zote za upili nchini. Wanafunzi wanaopata alama za chini katika mtihani wao wa darasa la nane hujiunga na shule za harambee, shule za biashara au kuacha shule. Vifaa katika shule hizi si vizuri kama vile vya shule zinazofadhiliwa na serikali, na mara nyingi hukosa vitabu, walimu waliohitimu, madawati n.k..

Shule nyingi za binafsi huwa na mfumo wa elimu ya Uingereza, ukifuatiwa na A-levels au Baccalaureate ya kimataifa, licha tu ya chache zinazofuata mfumo wa Marekani. Shule chache za binafsi hufuata mfumo wa KCSE kando ya mifumo ya kigeni wakiwapa wanafunzi kuchagua ni upi wa kufuatwa. Kwa mfano, Shule ya Saint Mary's, Nairobi.

Mfumo wa kutuza Gredi za KCSE

Grade A A - B + B B - C + C C - D + D D - E
Points 12 11 10 9 8 7 6 5 4 3 2 1

Gredi ya wastani hutegemea jinsi mwanafunzi hupita masomo haya nane. Endapo mtahiniwa atafanya zaidi ya masomo manane, gredi ya wastani itategemea masomo manane ya kwanza anayopita vyema zaidi. Kujiunga na chuo kikuu hutegemea masomo manane yanayopitwa zaidi na jinsi masomo fulani yamepitwa kutegemea kozi ya shahada fulani. Kwa mfano:

Somo Kundi Gredi Pointi
Kiingereza 1 B + 10
Kiswahili 1 A - 11
Hesabu 1 A 12
Historia na Serikali 3 B 9
Jiografia 3 A - 11
Fizikia 2 B + 10
Kemia 2 B - 8
Biolojia 2 A - 11

Jumla ya pointi ni 81.

Gredi ya wastani ni 81 na ukiigawa mara 8, ni sawa na 10.1 (hii ni karibu sawa na pointi10.0) ambayo ni B+ kwa mujibu wa mfumo wa gredi. Mwanafunzi apataye gredi kama hii hufaulu kujiunga na mojawapo ya vyuo vya umma kwa kupata gredi nzuri. Taasisi za mafunzo, vitivo na idara huamua mahitaji ya kimsingi ya kujiunga navyo.

Wanafunzi wanaopata gredi ya C+ hufaulu kusomea kozi ya shahada fulani katika chuo kikuu. Kwa sababu ya ushindani mkubwa na nafasi chache katika vyuo vikuu, wale wanaopata gredi ya B na wakati mwingine B- na zaidi huchukuliwa kusomea shahada mbalimbali katika vyuo vya umma na hufaidi kwa kulipa karo iliyotolewa ruzuku na serikali. Wale wengine hujiunga na vyuo vikuu vya kibinafsi au na vyuo vya kati.

Jambo la kushangaza ni kuwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vya umma kupitia J.A.B. hutegemea jumla ya nafasi za kulala zinazopatikana katika vyuo vyote vya umma. Hata hivyo wanaokosa nafasi hizi, ingawa walipata gredi za chini zaidi za kujiunga na vyuo vikuu C+ au C, wakiwa na cheti cha diploma fulani husajiliwa kupitia mpango wa kujilipia karo katika vyuo vikuu (Module II) ikiwa wanaweza kujilipia karo yote ya kozi husika.

Jambo hili limezua mjadala mkali huku watu wakiuliza sababu na uadilifu wa kuwafungia nje wanafunzi waliofaulu kujiunga na vyuo vya umma kisha kuwasajili wanaotoka kwa familia zenye uwezo wa kifedha.

Taasisi za Elimu[hariri | hariri chanzo]

Hizi ni taasisi zinazotoa elimu ya juu kwa miaka miwili au mitatu katika viwango vya Cheti, Diploma na Diploma ya juu ya kitaifa. Taasisi hizi hutoa mafunzo ya kiufundi kwa kutumia ujuzi wa mikono katika nyanja mbalimbali kama vile uhandisi, sayansi ya madawa, sayansi ya kompyuta n,k. Zinajumuisha vyuo vya mafunzo ya ualimu (TTCs), Taasisi za mafunzo ya udaktari nchini Kenya (KMTC), Kenya Polytechnic, Mombasa Polytechnic, Eldoret Polytechnic, Tasisi ya mafunzo ya utangazaji na nyingine nyingi. Taasisi hizi zote huanzishwa na miswada mbalimbali ya bunge.

Vyuo vya Umma[hariri | hariri chanzo]

Chuo kikongwe zaidi nchini Kenya ni Chuo Kikuu cha Nairobi. Vingine ni pamoja na vyuo vikuu vya Kenyatta, Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Egerton, Moi, Chuo Kikuu cha Maseno na Chuo Kikuu cha Masinde Muliro cha Sayansi na Teknolojia (zamani kilijulikana kama Chuo Kikuu cha Magharibi).

Habari zaidi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 1963 serikali ya Kenya iliahidi elimu ya msingi ya bure kwa watu wake. Ahadi hii haikufanikishwa hadi mwaka 2003. Wananchi wanatarajiwa kuchangia mfuko wa elimu kwa kulipia ada, kodi, na huduma za ajira. Baada ya kuchangia, wazazi wengi hawakuwa na pesa za kulipia elimu ya watoto wao na hatimaye waliachwa nje ya mfumo wa shule.

Walimu hushiriki mgomo mara nyingi kutokana na kutolipwa kwa mishahara yao. Walimu walihusika na kukusanya ada ya malipo kutoka kwa mwanafunzi, huku mishahara yao kushikiliwa hadi ada zote zilipokusanywa. Watoto wengi walikuwa wanalazimika kuacha shule tu kwa sababu hawakuweza kumudu gharama hii. Walimu mara nyingi walikuwa wakiwatuma watoto nyumbani wakati wa mitihani ya mwisho ili iwe shinikizo kwa wazazi kulipa ada ya shule.

Kwa sasa elimu ni bure, mahudhurio yameongezeka na kuna uhaba wa walimu na madarasa na watoto kutopata makini kutokana na ukosefu wa walimu wa kutosha inayotokana na msongamano wa wanafunzi madarasani. Hii ni matokeo ya watoto wote wanaohudhuria ambao hapo mwanzo hawakuweza kumudu ada ya shule, na watoto wanaotolewa shule za kibinafsi zenye hadhi ya chini ili kujinufaisha na ya elimu ya bure. Hii imejenga mahitaji kwa shule za kibinafsi zenya gharama ya chini ambazo wazazi wanaweweza kumudu kulipa ada kuwatutuma watoto wao ili kujifunza katika mazingira yaliyo bora.

Baadhi ya watu wanaamini kwamba msongamano katika mashule ni changamoto kwmba pana haja ya kuandaa mafunzo ya kiufundi zaidi ili kujenga njia mbadala kwa ajira.

Kenya ilianzisha mfumo wa sasa wa 8-4-4 mnamo mwaka wa 1985. Hii ina maana kwamba darasa la kwanza hadi la nane ni katika shule ya msingi, darasa la hadi kumi na mbili katika sekondari(Kidato cha kwanza hadi nne), na kisha wahitimu kutumia miaka minne katika chuo kikuu. Mfumo wa 8-4-4 iliundwa kusaidia wale wanafunzi ambao hawana mpango wa kuendeleza elimu ya juu. Umesaidia kupunguza viwango vya wanafunzi wanaoacha shule na kuwasaidia wale wanaoachia shule za msingi kupata ajira.

Ukuaji wa sekta ya elimu nchini Kenya umezidi matarajio. Baada ya chuo kikuu cha kwanza kuanzishwa mnamo mwaka wa 1970, vingine vitano vilitengenezwa. Mahitaji ya elimu ya juu imesababisha kuanzishwa kwa vyuo vikuu vya kibinafsi.

Vifaa katika baadhi ya vyuo vikuu vya umma ni ya hali ya chini hivi kwamba wale wa miaka ya juu hutumwa nyumbani kwa muda ili kuwapa nafasi wanafunzi wageni wanapojiunga na chuo kikuu. Vyuo vikuu, kama shule za msingi, vina ukosefu wa fedha ambazo zinazohitajika. Kuna ukosefu wa tarakilishi ya mafunzo, na maaabara ni ndogo na hazina vifaa vya kutosha. Baadhi ya wanafunzi huamua kulipa gharama ya juu kidogo ili kujiunga na vyuo vikuu vya kibinafsi kwa sababu hawataki kujihusisha na ushindani wa kutafuta nafasi za kujiandikisha. Pia, vyuo vikuu vya kibinafsi huwa na vifaa bora na maabara ya tarakilishi ya hali ya juu.

Serikali ya Uingereza inaipatia Kenya msaada wa shilingi bilioni saba (Dola milioni tisini na saba za Marekani) kusaidia kuboresha mfumo wa elimu ya bure. Fedha za ziada zitatumika kuboresha mipango ya afya katika shule zote. Pia, zitatumika katika ununuzi wa vitabu vya kusomea. Fedha hizi zitakwenda pia kupanua elimu ya shule ya upili na vyuo vikuu. Pia kutakuwa na ujenzi wa madarasa na uboreshaji wa vifaa vya ya maji pamoja na usafi wa mazingira.

Ingawa Kenya ina vyuo vikuu yake, baadhi ya wazazi huchagua kupeleka watoto wao katika nchi mbalimbali za kigeni. Wengi wanaamini kwamba Uingereza ina vyuo vikuu bora, na kwamba itakuwa fursa kubwa kwa watoto wao kuhudhuria chuo kikuu huko. Vyuo vikuu vya Kenya pia ni vigumu zaidi kujiunga navyo kutokana na mahitaji makubwa sana ya elimu ya juu na kuwepo kwa nafasi chache kwa wanafunzi kujiunga navyo.

Serikali ya Kenya ingawa kwa mwendo wa kobe, inajizatiti kufanya elimu nchini Kenya kuwa bora zadi. Miaka kumi na miwili ya kwanza ya shule sasa yanatolewa bure, japo hii ina imechangia suala la msongamano mashuleni; jambo linalohitaji kushughulikiwa kwa haraka. Ufadhili kutoka Uingereza utasaidia kujenga upya baadhi ya shule na hii itachangia kuboresha mazingira ya kujifunza.

Shule za binafsi[hariri | hariri chanzo]

Shule za binafsi nchini Kenya kwa ujumla huhudumia watu wa tabaka ya kati na ya juu. Nyingi ni ya mashirika ya kidini tofauti tofauti kama vile Oshwal Academy ambayo inamilikiwa na kusimamiwa na OERB (jamii ya Oshwal - Wakenya wenye asili ya kihindi wanaofuata dini ya Jainism); Katoliki (Saint Mary's School Nairobi), Wamisionari (Rift Valley Academy) na za Kiislamu (Aga Khan Academy). Mashirika haya kwa ujumla hufadhili shule hizo, na kwa kawaida hakuna upendeleo wa kidini au wa njia yoyote ile katika kuwachukua wanafunzi na uendeshaji wa shule.

Shule nyingi za binafsi nchini Kenya zinapatikana kakita jiji za Nairobi na Mombasa, huku shule za bweni zikipatikana sehemu ya mashambani au viungani mwa miji. Hii ni sambamba na mila ya familia za Uingereza za tabaka ya juu na juu ya kati kuwatuma watoto wao shule za bweni za gharama kubwa ambazo zina nafasi ya kutosha na vifaa. Shule zenyewe zinafanana na shule za umma za Uingereza, huku shule nyingi za kibinafsi jijini Nairobi aidha kuzingatia mfumo wa shule za umma, k.m. Brookhouse School, au kuwa shule za umma chini ya utawala wa kikoloni, k.m. Saint Mary's School, Nairobi na Kenton College.|Uingereza, huku shule nyingi za kibinafsi jijini Nairobi aidha kuzingatia mfumo wa shule za umma, k.m. Brookhouse School, au kuwa shule za umma chini ya utawala wa kikoloni, k.m. Saint Mary's School, Nairobi na Kenton College.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Standard - World's oldest pupil, Stephen Maruge, dies Archived 13 Januari 2015 at the Wayback Machine. 15 Agosti 2009

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]