Richie Spice

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Richie Spice
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaRichell Bonner
Amezaliwa8 Agosti 1971 (1971-08-08) (umri 52)
AlaVocals

Richie Spice (amezaliwa na jina la Richell Bonner mnamo 8 Septemba 1971 mjini Rock Hall, St Andrew nchini Jamaika) ni msanii wa Reggae. [1]

Richie Spice ni mwanachama wa vuguvugu la RASTAFARI. Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni kama, "Youth Dem Cold", "Groovin 'My Girl", "Earth A Run Red", "Marijuana" na "The Plane Land".

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Wimbo wa kwanza wa kijamaika wa Spice "Killing a Sound" ulikuwa umetayarishwa na Dennis "Star" Hayes. Hii ilifuatiwa na "Shine" na mtayarishaji / mwanamuziki Clive Hunt. Spice pia alijiunga na Hunt kwa albamu yake ya kwanza kutumia lebo la Island Jamaica ambapo alikuja na wimbo wake maarufu wa kwanza "Grooving my girl". Dada yake, Bridgett Bonner kwa Bonner Productions Ltd, alipanga albamu yake ya pili. Albamu ilikuwa na nyimbo kama "Earth a Run Red", "Living Ain't Easy", Nchi ya Jamaika "Time So Rough", na "Grooving My Girl" na mengine mengi.

Baada ya kupata umaarufu katika katikati ya miaka ya 1990, Spice ameigiza katika sherehe kuu hasa Reggae Sun Splash (kwa heshima ya Bob Marley), White River Reggae Bash, Rebel Salute na mengine mengi. Spice amefungua vionyesho kwa waimbaji kama Chaka Demus na Pliers, Spanner Banner na Rita Marley katika ziara mbalimbali za Ulaya na Marekani 1996-1997.

Yeye tena alizuru Amerika ya Kaskazini Mashariki kuanzia Juni hadi Septemba 2001. Umaarufu wake uliongezeka na ukampa nafasi katika kumbi mbalimbali. Miradi yake ya hivi karibuni ni pamoja maonyesho ya Sting yaliofanyika katika Jam World St Catherine (26 Desemba 2002) na Sting Miami (Machi 2003).

Pia hivi majuzi, ugeuzi wa moja wa nyimbo zake maarufu zaidi, "Marijuana" na Coki wa Digital Mystikz, iliyogeuzwa jina ikaitwa "BURNIN'" imemjengea jina na kumsaidia kusikika huko nje hata huko Uingereza. Wimbo halisi wa "Marijuana" pia unaonekana katika "These are Serious Times" mkusanyiko wa nyimbo za Reggae za kisasa wa Studio ya XL.

Wimbo wake 'Youths Dem Cold' ulichezwa kwa Redio ya kipindi cha Grand_Theft_Auto_IV_soundtrack # Massive_B_Soundsystem_96.9 katika GTA IV

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Richie Spice at Zanzibar. Washington Post. Iliwekwa mnamo 2008-10-05.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Richie Spice kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.