Brazzaville

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Jiji la Brazzaville
Nchi Jamhuri ya Kongo
Brazzaville.
Kinshasa, Brazzaville na mto Kongo.

Brazzaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo. Una wakazi 2,308,000 (mwaka 2019) ambao ni sawa na 40% ya wananchi wote.

Uko kando ya mto Kongo ukitazamana na mji wa Kinshasa ng'ambo ya mto.

Brazzaville una bandari kwenye mto Kongo na mwanzo wa reli kuelekea pwani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jina la Brazzaville limetokana na Mfaransa Pierre Savorgnan de Brazza aliyenunua hapa ardhi kutoka kwa chifu Makoko na kujenga kituo kilichokua na kuwa mji baadaye.

Tangu mwaka 1898 Brazzaville ulikuwa mji mkuu wa Kongo ya Kifaransa ukawa na wakazi 5,000 mnamo 1900 walioongezeka kuwa lakhi moja mwaka 1950.

Mwaka 1940 Brazzaville ulikuwa kwa muda mfupi mji mkuu wa Ufaransa Huru yaani Ufaransa usio chini ya Ujerumani hadi kuhamia kwa serikali hiyo kwenda Algiers.

Vitabu[hariri | hariri chanzo]