Tony Almeida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tony Almeida
muhusika wa 24

Carlos Bernard kama Tony Almeida
Imechezwa na Carlos Bernard
Misimu
1, 2, 3, 4, 5, 7
Maelezo

Anthony "Tony" Almeida ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24[1]. Uhusika ulichezwa na Carlos Bernard. Almeida, ni mmoja kati ya watu ambao Jack Bauer bado anawaamini hadi hapo ilipofikia umauti wake katika Msimu wa Tano.[2] Tony anaonekana akifa mikononi mwa Bauer katika sehemu ya kumi na tatu ya msimu tano, lakini alifufuliwa baada ya dakika kumi kwa kutumia sindano ya hypothermic, na kurejea katika msimu wa saba.

Katika uhusika[hariri | hariri chanzo]

Tony Almeida alizaliwa mjini Chicago, Illinois, mnamo mwaka wa 1973.[3] Ana stashahada ya Computer Science na Engineering alioipata katika Chuo Kikuu cha Jimbo la San Diego na Master's degree ya Computer Science kutoka katika Chuo Kikuu cha Stanford. Alishawahi kutumikia kama Luteni katika Jeshi la Maji la Marekani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ken Tucker, “24: Mondays, 9 p.m., premiering Sunday, Jan. 11, at 8 p.m.,” Entertainment Weekly 1030 (16 Januari 2009): 56.
  2. Carr, Coeli. "Surviving So Jack Bauer Can Live Another Day", The New York Times, 15 Januari 2006. Retrieved on 2008-07-07. 
  3. Cerasini, Marc (2003). 24: The House Special Subcommittee's Findings at CTU (First ed.). Harper Collins. p. 71. ISBN 0-06-053550-4. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]