National Alliance Party of Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

National Alliance Party of Kenya (NAK) ilikuwa maungano ya vyama vya kisiasa nchini Kenya yaliyoanzishwa kabla ya uchaguzi wa rais na bunge wa mwaka 2002. Kusidi lake lilikuwa kuunganisha vikundi vyote vilipinga utawala wa rais Daniel arap Moi na chama chake cha KANU. NAK ilikwisha mwaka uleule katika ushirikiano wa NARC.

Chanzo cha NAK[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha NAK kilikuwa maarifa ya miaka iliyotangulia ambako KANU ilishinda uchaguzi kama bila kuwa na kura nyingi kabisa lakini kutokana na uhaba wa umoja upande wa upinzani. Baada ya kufarakana kwa Forum for the Restauration of Democracy 1992 vyama vyote vya upinzani vilikuwa na tabia za kikabila vikiwa na msingi kati ya moja ya makabila makubwa tu.

Hivyo viongozi wa vyama vikubwa vya upinzani walipatana ushirikiano. Walioongoza hasa walikuwa:

Waliungwa mkono na vyama vingine vidogo jumla 13. Mwanzoni walitumia jina la "National Alliance for Change" (NAC) lakini chama kilitwa rasmi NAK.

Mapatano ya NAK[hariri | hariri chanzo]

Vyama vya NAK vilipatana kukaribia uchaguzi na Kibaki kama mgombea wa urais, Wamalwa kama makamu wake na Charity Ngilu kwa cheo cha Waziri Mkuu kilichopangwa kuanzishwa baada ya marekebisho ya katiba.

Kuingia katika Rainbow[hariri | hariri chanzo]

Miezi michache kabla uchaguzi kulitokea farakano kubwa katika KANU. Kundi la Raila Odinga iliondoka pamoja na wanaKANU wa miaka mingi waliosikitika uteuzi wa Uhuru Kenyatta kama mgombea wa urais upande wa KANU.

Waliotoka waliunda chama cha Liberal Democratic Party of Kenya (LDP) na kutumia alama ya pinde (rainbow).

Vikundi vyote viwili vya NAK na LDP vikaamua kuungana kwa jina la "National Rainbow Coalition". Vyama vya NAK havikushikamana tena pamoja katika uchaguzi lakini vyama vyote vilipatana kuepukana na mashindano kato yao hata vikipeleka wagombea kwa jina la kila chama.