Ukambani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Ukambani nchini Kenya

Ukambani ni sehemu ya kusini ya uliokuwa Mkoa wa Mashariki nchini Kenya. Mazingira yake huona ukame wa mara kwa mara pamoja na njaa inayokuja sambamba nayo.

Eneo la Ukambani linaanza upande wa mashariki wa Nairobi na kuendelea hadi Tsavo; kwa mtazamo tofauti ni eneo kati ya Embu na mpaka wa Tanzania. Jumla ni Km² 41,000 ambazo hukaliwa na watu milioni 4, wengi wakawa Wakamba.

Kaunti za Ukambani ni hasa Machakos, Kitui na Makueni ambazo kati yake Kitui ndiyo kubwa zaidi na Machakos ile yenye wakazi wengi zaidi.