Ziwa la oksbau
Mandhari

Ziwa la oksbau (Kiingereza: oxbow) ni ziwa au bwawa lenye umbo la U ambalo hutokea wakati mzunguko mpana wa mto unapokatwa, na kutengeneza sehemu ya maji iliyotenganika. Neno la Kiingereza "oxbow" linaweza pia kurejelea mzingo wenye umbo la U katika mto au kijito, uwe umekatwa kutoka kwenye mkondo mkuu au la.[1][2] Linapata jina lake kutoka "oxbow" ambayo ni sehemu ya nira ya ng'ombe kwa ajili ya kuvutia jembe au gari la kukokotwa.
Katika Texas Kusini, maziwa ya aina hiyo yaliyoachwa na Mto Rio Grande huitwa resacas. Nchini Australia, maziwa ya oksbau huitwa billabongs.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Oxford Languages". Oxford Languages (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-06-11.
- ↑ https://www.merriam-webster.com/cgi-bin/dictionary?book=Dictionary&va=oxbow
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ziwa la oksbau kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |