Zerubabeli


Zerubabeli (kwa Kiebrania: זְרֻבָּבֶל, Zerubbāḇel, yaani mbegu ya Babeli [1][2]) alikuwa Myahudi wa karne ya 6 KK, mwana wa Shealtieli[3] na mjukuu wa mfalme Yekonia[4]. Alifanywa na mfalme Koreshi II wa Uajemi kuwa gavana wa Yuda [5][6][7], akawa hivyo mtu wa mwisho wa ukoo wa Daudi kushika madaraka ya kisiasa, ingawa si kama mfalme [8].
Ndiye aliyeongoza kundi la kwanza la waliorudi Yerusalemu baada ya uhamisho wa Babeli[9] mwaka 538 KK[10]. Ndiye pia aliyeanzisha ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu[11] lililokuwa limebolewa na Nebukadreza II mwaka 586 KK. Matarajio mbalimbali yalikuwepo juu yake [12], lakini hayakutimia mpaka alipotokea Yesu Kristo ambaye Injili ya Mathayo (1:12) na ile ya Luka (3:27) zinasema wazi kwamba alitokana na Zerubabeli.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Finkelstein, Israel; Silberman, Neil Asher (2006). David and Solomon: in search of the Bible's sacred kings and the roots of the Western tradition. New York: Free Press. ISBN 0-7432-4362-5.
- ↑ "Zerubbabel." Encyclopaedia Judaica online. 2nd ed. Macmillan Reference, Detroit, USA, 2007. Gale Virtual Reference Library. Retrieved 6 Dec. 2010.
- ↑ Kitabu cha Ezra 3:2,8; 5:2; Neh 12:1; Kitabu cha Hagai 1:1,12,14
- ↑ Silverman, Jason M. (2019). "Zerubbabel". Katika Stuckenbruck, Loren T.; Gurtner, Daniel M. (whr.). T&T Clark Encyclopedia of Second Temple Judaism. Juz. la 2. Bloomsbury Publishing. uk. 840. ISBN 978-0-567-66095-4.
- ↑ Hag 1:1
- ↑ Schulz, Sarah (Aprili 2023). "Between History and Theology—Zerubbabel and Nehemiah as Governors of Judah from the Perspective of Literary History". Religions. 14 (4: 531, Special Issue "The History of Literature and Theology in the Hebrew Bible"). MDPI. doi:10.3390/rel14040531.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kessler, John (2006). "Haggai, Zerubbabel, and the Political Status of Yehud: The Signet Ring in Haggai 2:23". Katika Michael Floyd; Robert D. Haak (whr.). Prophets, Prophecy, and Prophetic Texts in Second Temple Judaism. T & T Clark Int'l. ku. 102–119 (see 104). ISBN 978-0-567-02780-1.
- ↑ Kitabu cha Yeremia 22:30; Hag 2:"3
- ↑ Ezr 2:1–2, 64; 3:8; 5:2; Neh 12:1
- ↑ Janet E. Tollington, Tradition and Innovation in Haggai and Zechariah 1–8 (Sheffield, England: Sheffield Academic Press, 1993), 132.
- ↑ Diana Edelman. The Origins of the 'Second' Temple: Persian Imperial Policy and the Rebuilding of Jerusalem. (Oakville, CT, Equinox Publishing Ltd, 2005. 2.
- ↑ Kitabu cha Zekaria 1:1-14
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]
- Easton's Bible Dictionary: Zerubbabel
- Jewish Encyclopedia: Zerubbabel
- GOTHOD- Zerubbabel Archived 2021-08-04 at the Wayback Machine Hebrew University of Jerusalem
| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zerubabeli kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
