Nenda kwa yaliyomo

Zekaria wa Israeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Zekaria alivyochorwa katika "Promptuarii Iconum Insigniorum" mwaka 1553.

Zekaria wa Israeli (kwa Kiebrania זְכַרְיָה, Zəḵaryā) alikuwa mwana na mwandamizi wa Yeroboamu II kama mtawala wa Ufalme wa Israeli, ambao aliuongoza miezi 6 tu hadi alipouawa na kapteni wake Shalumu aliyejifanya mfalme badala yake (752 KK hivi).

Biblia inamhukumu kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15:8-12.

    Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Zekaria wa Israeli kama habari za maisha au kazi yake?
    Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.