Nenda kwa yaliyomo

Zehira Houfani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Zehira Houfani-Berfas (Kiarabu: زهيرة حوفاني برفاس; alizaliwa 16 Septemba 1952) ni mwandishi kutoka Algeria anayefanya kazi kwa lugha ya Kifaransa na anaishi nchini Canada. Inaaminika kuwa huenda alikuwa mwanamke wa kwanza kuchapisha riwaya ya upelelezi nchini Algeria.

Zehira Houfani alizaliwa tarehe 16 Septemba 1952 huko M’Kira, Algeria.[1] Riwaya yake ya kwanza ilifahamika kwa jina la Les Pirates du désert yenye tafsiri : Maharamia wa Jangwa iliyochapishwa mwaka 1986. Hadithi hiyo iliwekwa katika mji wa Tamanrasset kusini mwa Algeria na iliandikwa kwa mtindo wa waandishi maarufu wa riwaya za upelelezi kama Dashiell Hammett na Raymond Chandler.

Wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Algeria, aliacha kuandika riwaya za upelelezi. Mwaka 1994, alihamia kuishi nchini Canada.Pia alifanya kazi kama mwanaharakati wa amani.Alitembelea Iraq kurekodi madhara na vifo vya raia wakati wa Vita vya Iraq, na pia alidai rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, ajiuzulu.

  1. "Zehira Houfani Berfas". Babelio (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2026-02-04.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zehira Houfani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.