Zamaradi Mketema

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

'

Zamaradi Mketema
Amezaliwa(1985-10-04)Oktoba 4, 1985
Dar es Salaam, Tanzania
NchiTanzania
Kazi yakeMtangazaji
Watoto3


Zamaradi Mketema alizaliwa tarehe 4 Oktoba mnamo mwaka 1985.Ni mtangazaji wa redio na televisheni kutoka Tanzania aliyepata umaarufu kwa utangazaji wake kwenye kipindi cha Take One kilichokuwa kikirushwa na kituo cha televisheni cha Clouds. [1].

Maisha na elimu

Zamaradi Mketema alizaliwa Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye kuanza shule ya msingi Muhimbili. Alianza masomo ya Sekondari katika Shule ya Kiislam ya Wasichana huko Kunduchi, kisha kujiunga na Shule ya (St Mary’s International Mbezi Beach) ambapo alimaliza kidato cha nne. Badaye alijiunga na Green Acres kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita, hata hivyo hakuweza kumaliza shuleni hapo, alihama na kujiunga na Shule ya (Hillside High International School) iliyopo Bunamwaya, Uganda na baadae kurudi Tanzania alipomaliza kidato cha sita.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Mt. Augustino tawi la Mwanza alipokuwa akichukua Shahada ya kwanza ya Uhusiano wa kijamii. Chuoni aliweza kushiriki mashindano ya Miss Mwanza mwaka 2007 na kuweza kushika nafasi ya kwanza lakini hakuweza kuendelea na mashindano hayo ya urembo baada ya kukatazwa na Baba yake mzazi kwa sababu za kidini. [2].

Kazi

Zamaradi Mketema alianza kuwa mtangazaji kwenye kituo cha Televisheni cha C2C kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008.

Mbali na utangazaji pia alitoa filamu ya kwanza iliyoitwa Nzowa, kisha mwaka 2014 alifanikiwa kutoa filamu yake ya Kigodoro aliyowashirikisha wasanii wengi wa Tanzania na kufanikiwa kushinda kwenye tuzo za watu kama filamu bora ya mwaka, lakini pia alitengeneza documentary inayofahamika kama neno la mwisho inayohusu maisha ya marehemu Steven Kanumba ambayealikuwa muigizaji mkubwa Tanzania. [3].

Mahusiano

Zamaradi ana watoto watatu, kati ya hao wawili aliwapata kabla hajafunga ndoa na Ruge Mutahaba, na mmoja alimpata kwenye ndoa iliyofungwa mwaka 2017 na Mpwa wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, jijini Dar es Salaam. [4].

Marejeo

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zamaradi Mketema kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.