Zaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa kutaja watoto wa wadudu angalia makala ya lava

Zaha (pia: lava; ing. lava) ni mwamba ulio katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa dunia mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "magma" badala ya zaha. Sawa na magma yenyewe zaha inaweza kuwa nzito kama uji-uji au nyepesi kama maji-maji. [1] .

Zaha inatoka nje kwa kawaida wakati wa mlipuko wa volkeno. Inaweza kutoka pia katika ufa kwenye ganda la dunia.

Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600°C hadi 1200 °C. Ndani ya shimo la kasoko ya volkeno lava inaweza kukaa kama ziwa la kuchemka.

Ikitoka nje ya kasoko inaweza kuwa kama mto wa moto. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.

Ikipoa inaganda na kuwa mwamba imara

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. (2001) Earth Science. Holt, Rinehart and Winston, Austin, Texas. ISBN 0-03-055667-8.