Yusuph Kileo
| Yusuph Kileo | |
|---|---|
| Amezaliwa | 7 Septemba 1989 |
| Utaifa | Mtanzania |
| Mhitimu | Dar es Salaam Institute of Technology Chuo Kikuu cha Staffordshire Chuo Kikuu cha Mashariki ya Mediterania (Eastern Mediterranean University - EMU) |
| Kazi yake | Mtaalamu wa Usalama wa Mtandao na Uchunguzi wa Kidijitali (Cyber Security and Forensics) |
| Miaka ya kazi | 2009-hadi sasa |
Yusuph Kileo (amezaliwa Septemba 7, 1989) ni mtaalamu wa Usalama wa mtandao na Uchunguzi wa makosa ya kidijiti (Digital Forensics). Kileo amekua katika tasnia ya usalama mtandao kwa muda mrefu na kua chachu ya kuimarisha sekata hii ya usalama mtandao katika maeneo mengi. Huongoza na kuratibu mijadala mbalimbali kuhusu elimu ya usalama , hatari na uhalifu wa mitandaoni, pamoja na kutoa maoni kwenye vyombo vya habari, runinga, redio, magazeti na katika mitandao ya kijamii[1]. Juhudi zake zinaenea katika uhamasishaji wa usalama kwa watumiaji mitandao hususan katika kampeni ya Ulinzi wa Mtoto Mtandaoni ya nchini Tanzania aliyoiasisi na kuzindua rasmi mwaka 2024[2][3][4].
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Alisoma chuo cha teknolojia cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) na baadaye alijiunga katika Idara ya Uhandisi akibobea katika ufundi wa kompyuta.
Mnamo mwaka 2009 mpaka 2012 alisoma Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Staffordshire, Uingereza, ambako alipata Shahada ya Sayansi katika Usalama wa Kompyuta, huku mradi wake wa mwisho ulikua umebebwa na kichwa cha habari "Mfumo Mahiri wa Udhibiti wa Ufikiaji (Intelligent Access Control System).”[5]
Mwaka 2015 alipata Shahada ya Umahiri katika Teknolojia ya Habari kutoka Chuo kikuu cha Eastern Mediterranean, akiwa amejikita katika Usimamizi wa Miradi na Hatari katika Teknolojia ya Habari.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Yusuph alikuza ujuzi wake wa Teknolojia ya Habari alipofanya kazi na Brand East Africa mwaka 2006. Kisha, mnamoi mwaka 2008 alijiunga na Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL), ambapo alianza kupendezwa na nyanja ya usalama wa mtandao.
Mwaka wa 2010, alijiunga na idara ya IT ya Deloitte. Mwaka wa 2012, alishiriki kama mtaalamu wa Usalama wa Mtandao na Uchunguzi wa Kimtandao kwa Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai ya Polisi, chini ya Ofisi ya Uchunguzi wa Kisasa (Forensics Bureau). Huko, alifanya mafunzo na kutoa maelezo kuhusu changamoto za usalama wa mtandao nchini Tanzania. Kama mwanasayansi wa Teknolojia ya Habari, anazingatia utatuzi wa matatizo, usanikishaji, uchunguzi, na ufumbuzi wa kiufundi[6][7].
Pia, amefanya kazi kama mtangazaji wa redio (Uhuru FM) na mkufunzi katika mashirika ya BTG US na Tanzania kwa ujumla.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]Yusuph Kileo amepokea tuzo na kutambuliwa kwa mchango wake katika nyanja ya Usalama wa mtandao, Uchunguzi wa Kimtandao, na Utawala wa Mtandao (Internet Governance). Hapa kuna baadhi ya tuzo alizotunukiwa:
- Tuzo ya U-EDGE (Outstanding Achievement Award) Alitunukiwa kwa Uongozi na Utaalamu katika masuala ya teknolojia na usalama wa mtandao. Hii aliipata baada ya alipomaliza masomo yake ya Shahada ya Kwanza katika Usalama wa Kompyuta kwenye Chuo Kikuu cha Staffordshire, Uingereza.
- Tuzo za Utambuzi kutoka Serikali ya Tanzania Alitunukiwa tuzo hii na Serikali ya Tanzania baada ya mchango wake katika Idara ya Uchunguzi wa makosa ya Jinai akiwa kama mtaalamu wa Uchunguzi wa uhalifu wa mitandaoni ( Cybercrime ). Alitoa mafunzo na mbinu za kisasa za kukabiliana na uhalifu wa kidijitali nchini Tanzania.
- Utambuzi katika ICANN na AfICTA[8] Alitunukiwa tuzo hii akiwa kama Mwanabodi wa AfICTA na Mwakilishi wa ICANN, amepewa heshima kwa kushiriki katika mijadala ya kimataifa kuhusu usalama wa mtandao na utawala wa internet. Ambapo alitoa mchango katika DNS Abuse Working Group na kamati za kifedha za ICANN[9][10].
- Tuzo za Mafunzo na Ushiriki wa Jamii Alitunukiwa tuzo hii kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi, maafisa wa serikali, na wataalamu wa Teknolojia ya Habari katika mikutano ya kitaifa na kimataifa [11].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Vijana, Wanafunzi na Hatari ya Kufanyiwa Uhalifu Mtandaoni". blog.maelezo.go.tz. Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ "Mikakati kudhibiti athari za mitandao kwa watoto yaja – HabariLeo" (kwa American English). 2023-05-01. Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ "MoCDGWSG | RAS MOROGORO AHIMIZA USHIRIKIANO KWA WATENDAJI WA SERIKALI KATIKA USALAMA WA MTOTO MTANDAONI". www.jamii.go.tz. Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ "Guardians at the digital gate: Safeguarding children in the age of mobile technology | The Guardian". www.ippmedia.com. Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ "Yusuph Kileo's Speaker Profile". sessionize.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-05-13.
- ↑ Staff Writer (2015-05-14). "Africa's critical infrastructure vulnerable to attack". ITWeb (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ "Yusuph Kileo News | ITWeb Africa". itweb.africa. Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ "Finance Committee". www.icannbc.org. Iliwekwa mnamo 2025-05-14.
- ↑ AfICTA (2016-10-20). "Yusuph Kileo". AfICTA (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2025-05-13.
- ↑ https://www.bizconst.org/assets/docs/newsletters/2022_ICANN73-BC-NEWSLETTER.pdf
- ↑ "Yusuph Kileo akwaa tuzo ya TEHAMA", BBC News Swahili, iliwekwa mnamo 2025-05-13
| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |